HABARI ZA LEO
6/08/2012
ASKARI ALIYEWALIPUA WENZAKE MOROGORO ADAIWAKUJINYONGA
Mwili wa Donald Mathew ‘Dunga’ ukiondolewa mtini.
Barua ya Dunga kwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
ASKARI jasiri aliyejizolea sifa mkoani hapa kwa kitendo chake cha
kuwataja hadharani baadhi ya askari wenzake akiwashutumu kwa tuhuma
mbalimbali zikiwemo za kushirikiana na majambazi kufanya uharifu, Donald
Julius Mathew, mwenye namba ya jeshi la polisi F3276 amekufa akidaiwa
kujinyonga.
Mwili ya afande huyo ambaye ni maarufu mkoani hapa kwa jina la Dunga umekutwa ukiningin'ia juu ya mti eneo la Daraja la Shani ambalo liko katikati ya Mji wa Morogoro.
Dunga aliwalipua maafande zaidi ya sita ambao walihamishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema na yeye kuhamishwa mkoa wa Singida.
Hata hivyo, Dunga aligomea uhamisho huo akipinga watuhumiwa kutochukuliwa hatua.
Sababu alizotoa Dunga zinaelezwa katika barua aliyomwandikia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyoitoa kwa mtandao huu na ambayo tunaichapisha.
Mwili ya afande huyo ambaye ni maarufu mkoani hapa kwa jina la Dunga umekutwa ukiningin'ia juu ya mti eneo la Daraja la Shani ambalo liko katikati ya Mji wa Morogoro.
Dunga aliwalipua maafande zaidi ya sita ambao walihamishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema na yeye kuhamishwa mkoa wa Singida.
Hata hivyo, Dunga aligomea uhamisho huo akipinga watuhumiwa kutochukuliwa hatua.
Sababu alizotoa Dunga zinaelezwa katika barua aliyomwandikia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyoitoa kwa mtandao huu na ambayo tunaichapisha.
KOZI YA UTAWALA IMEFUNGULIWA RASMI NA RAIS WA TFF
Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amefungua rasmi Kozi ya Uongozi na
Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoanza leo Agosti
6 mwaka huu Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
Kozi hiyo ina
washiriki zaidi ya 30 itamalizika Agosti 11 mwaka huu na itaendeshwa na
Wakufunzi kutoka FIFA na imefunguliwa leo saa tatu asubuhi.
Wakufunzi hao
ni Barry Rukoro anayetoka Namibia, Henry Tandau (Tanzania) na Senka Kanyenvu
(Botswana).
YANGA WATUA BUNGENI KWA MBWEMBWE, SPIKA, WAZIRI MEMBE WAWAPONGEZA LAKINI RAGE AWAPIGA DONGO...!!
Wachezaji wa Yanga wakishangilia taji lao la ubingwa wa Kombe la Kagame hivi karibuni... kombe hilo limetambulishwa kwa wabunge mjini Dodoma leo |
Kikosi cha klabu ya Yanga kimetua kwa kishindo ndani
ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo na kuibua shangwe na nderemo
kutoka kwa wabunge mashabiki wa timu hiyo wakati wakitambulisha kombe walilotwaa
hivi karibuni la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu Kombe la
Kagame.
Baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu,
wachezaji wa Yanga walioongozana na mwenyekiti Yusuf Manji, Makamu
MwenyekitiClement Sanga, mjumbe wa bodi ya wadhamini, Mama Fatma Karume na
Francis Kifukwe walitambulishwa na bungeni na kupongezwa na Spika wa Bunge, Mhe.
Anna Makinda.
Kufuatia tukio hilo, wabunge waliripuka kwa shangwe na
bashasha tele, huku wale ambao wanafahamika kuwa ni mashabiki wa Simba, kama
Mhe. Ismail Aden Rage ambaye pia ni mwenyekiti wa wekundu hao wa Msimbazi,
wakionekana kushangilia vilevile, lakini kwa namna ya utani
zaidi.
Baada ya utambulisho wa msafara wa wachezaji wa Yanga,
wakiwamo nyota kama Haruna Niyonzima ‘Fabregas’, Hamis Kiiza na mfungaji bora
wa michuano ya Kagame, Said Bahanunzi, likaja tukio la kuonyeshwa kwa kombe
walilotwaa, la Kagame.
Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisimama na kombe
hilo, akaenda mbele na kulipunga hewani huku akilielekeza kila upande ili
wabunge wote wapate nafasi ya kuliona. Ushangiliaji wa kupiga meza ulitwaa
nafasi na kuufanya ukumbi mzima urindime.
Hata hivyo, katikati ya kushangilia huko, wabunge
wengi ambao ni mashabiki wa Simba, wakiongozwa na Rage, wakajibu mapigo ya
wapinzani wao wa jadi kwa namna ya kuchekesha zaidi baada ya kunyoosha juu
vidole vitano vya mkono; pengine wakikumbushia matokeo ya kichapo kikali cha
mabao 5-0 walichowapiga Yanga katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu ya Tanzania
Bara!
Baadaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Benard Membe akawapongeza Yanga wakati akisoma hotuba ya makadirio ya
mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha.
Membe ambaye pia ni mnazi wa Yanga, akasema kwamba
atakuwa hajatenda haki kama hatawapongeza Yanga ambao wamekuwa mabalozi wazuri
wa Tanzania kwa kutwaa ubingwa wa Kagame unaohusisha klabu bingwa za Afrika
Mashariki na Kati; na kwamba amefurahi kuwa ujio wao bungeni umekuja katika siku
mwafaka ambayo wizara yake inawasilisha bajeti ya mwaka ujao wa fedha.
Yanga walitwaa kombe la Kagame kwa mara ya pili
mfululizo baada ya kushinda 2-0 katika mechi yao ya fainali dhidi ya Azam
FC.
MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUTURISHA IKULU NDOGO MJINI DODOMA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tano
kutoka kulia) akijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika swala ya
Magharibi wakati wa hafla ya Futari aliyowaandalia na kushiriki nao pamoja
katika futari hiyo iliyoandaliwa Ikulu ndogo mjini Dodoma jana.
![]() | |||||
Makamu wa Rais, Dkt Bilal, akiagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi. |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,
baada ya hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma
jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana
na Waziri Maliasili na Utalii, Hamis Kagasheki, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya
waalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma
jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana
wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari,
iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana
wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari,
iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana
wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari,
iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana
na Mhe. Juma Kapuya, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya waalikwa katika hafla ya
futari iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana
wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari,
iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana
wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari,
iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana
TRAFIKI KUPANGWA MLIMA KITONGA ILI KUPUNGUZA AJALI ASEMA KAMANDA MPINGA
KUTOKANA na ajali za mara kwa mara zinazoendelea kutokea katika mlima wa kitonga katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga amekiagiza kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa kuwekwa askari wa kutosha wa usalama barabarani (Trafiki) katika mlima huo.
Akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com jana baada ya kutembelea eneo hilo la Kitonga na kushuhudia jinsi ambavyo mabasi ya abiria na malori ya mizigo yanavyopita kwa kasi bila tahadhari yoyote katika kona za mlima huo ambazo kimsingi ni kona kali ambazo madereva wanapaswa kuendeshwa kwa uangalifu wa hali ya juu.
Alisema kuwa kati ya maeneo yanayoongoza kwa ajali za mara kwa mara na kusababisha vifo vya watanzania ni pamoja na eneo hilo la mlima Kitonga hivyo bila kuwepo kwa mikakati ya haraka kutoka kikosi hicho cha usalama barabarani uwezekano wa kupunguza ajali hiyo bado utakuwa ni mdogo zaidi.
kamanda Mpinga alisema kuwa moja ya mikakati ambayo kikosi chake kilikuwa kikiitazama kuifanya kama njia ya kuepusha ajali eneo hilo ni pamoja na kukutana na wakala wa barabara mkoa wa Iringa (Tanroads) ili kuweka matuta katika eneo hilo ila mkakati huo baada ya kuufanyia utafiti wa kutosha wameona si njia nzuri ya kupunguza ajali kutokana na eneo hilo kuwa na mlima mkali hivyo wanahofu ukawa ni sehemu ya ajali hasa kwa magari yanayopandisha mlima huo.
Hivyo alisema mkakati rahisi ambao wanaona utasaidia kupunguza ajali za barabarani ni kukomesha matukio ya uharifu kwa madereva kuvamiwa na majambazi katika eneo hilo ni kuweka doria ya askari Trafiki ambao watatembea kwa miguu na wengine kufanya doria ya magari mara kwa mara katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na malori na magari yote ya abiria kukaguliwa kabla ya kuanza kushuka ama kupandisha eneo hilo la mlima na mteremkoa mkali wa Kitonga.
"Njia hii ya kukagua mabasi ya abiria na malori itasaidia kujua matatizo ya gari husika na iwapo litabainika kuwa ni bovu basi halitaruhusiwa kushuka wala kupanda eneo hilo la Kitonga hadi litakapo tegenezwa"
Kwani alisema kuwa ajali nyingi zinazotokea eneo hilo zinasababishwa na ubovu wa vyombo hivyo vya usafiri ama uzembe wa madereva kwa kutaka kuyapita magari mengine bila kutazama kona kali zilizopo katika eneo hilo.
Aidha alisema hata Tanroads mkoa wa Iringa inapaswa kuweza kuweka alama za kutosha za usalama barabara katika mlima huo ili kuwafanya madereva kuchukua tahadhari badala ya kuacha alama chache zilizopo kwa sasa.
MKUTANO WA CHADEMA LONDON
M4C LONDON
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA
MAENDELEO CHADEMA KINAPENDA KUWATANGAZIA WATANZANIA WOTE WAISHIO LONDON
NA SEHEMU ZA JIRANI KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO WA UFUNGUZI WA TAWI LA
CHADEMA LONDON. TAWI AMBALO LITAFUNGULIWA NA MHESHIMIWA GODBLESS LEMA.
UFUNGUZI HUO UTAFANYIKA THATCHED HOUSE PUB ILIYOPO BARKING SIKU YA JUMANNE 07/08/2012 SAA MBILI USIKU.
KATIKA MKUTANO HUO PIA WATACHAGULIWA VIONGOZI MBALIMBALI WA CHADEMA TAWI LA LONDON .
TUNAWAOMBA WANACHADEMA WOTE WAJITOKEZE KWA WINGI KUJA KUHUDHURIA TUKIO HILI LA KIHISTORIA.
Venue ; Thatched House Pub
RIPPLE ROAD, BARKING, ESSEX, IG11 9PG Kwa maelezo zaidi wasiliana na chacha thomas 0712689297
AJALI MBAYA YA MALORI YAUA WANNE KITONGA IRINGA
HUKU mkoa wa Iringa ukiwa umepewa hadhi ya kuwa mwenyeji wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani kwa mwaka huu ,mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda ashuhudia ajali mbaya iliyopelekea vifo vya watu wanne kufa papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana na kutumbukia bondeni katika mteremko wa mlima kitonga wilayani Kilolo katika barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam .
Hata hivyo dereva wa lori bovu ambalo lilikuwa limeegeshwa eneo hilo alipona katika ajali hiyo .
Akizungumza katika eneo la ajali mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga alisema kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia jana na kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T587 BGP aina la scania ambalo lilikuwa na mali mbali mbali za dukani lilikuwa limeharibika na kuegeshwa kando ya barabara hiyo kugongwa na lori lenye namba za usajili T T319 BDG aina ya Scania ambalo lilikuwa limebeba shaba kuligonga lori lililokuwa limeegesha kando ya barabara hiyo.
Mpinga alisema kuwa katika ajali hiyo watu wanne walikufa papo hapo na mmoja ambaye ni kijana alijeruhiwa vibaya na kuwa miongoni mwa waliokufa ni pamoja na mwanamke mmoja ambaye inasadikika ni mkazi wa wilaya ya kilolo aliyekuwa amepanda katika lori hilo .
Alisema kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha ni pamoja na utingo wa lori ambalo lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara hiyo ambalo lilikuwa limebeba mali za dukani ambaye alikuwa nje ya lori hilo akifanya mawasiliano ya simu na mwenzake na hivyo kugongwa na lori hilo la Shaba ambalo breck zilionyesha kuwa na matatizo.
Hata hivyo alisema kuwa pamoja na ajali hiyo kutokea Agosti 4 majira ya jioni ila zoezi la utoaji wa maiti ya dereva wa lori hilo lenye shaba bado ni gumu kutokana na mwili wa dereva huyo kubanwa vibaya ya tela la lori hilo lenye shaba .
Alisema kuwa kabla ya tela hilo lenye shaba kufunika kibini ya lori hilo kebini hiyo ilikatika na kutangulia korongoni na baada ya hapo tela lenye shaba kufuata nyuma na kutua juu ya kibini hiyo.
kamanda huyo alisema kuwa ajali hiyo imetokea wakati mkoa wa Iringa unataraji kuwa mwenyeji wa wiki ya nenda kwa usalama ambayo kitaifa itafanyika katika mkoa wa Iringa huku akiwataka madereva kuheshimu sheria za usalama barabarani kama njia ya kuepuka ajali kama hizo.
Aidha alisema kuwa kutokana na eneo hilo la mlima wa Kitonga kuendelea kuwa na eneo maarufu kwa ajili tayari mkakati umewekwa kwa ajili ya kuongeza ulinzi en eo hilo pamoja na kufanya doria za mara kwa mara za miguu ya magari kwa askari wa usalama barabarani ili kusaidia kupunguza ajali katika eneo hilo.
Alisema kuanzia sasa askari wa usalama barabara watawekwa eneo hilo ili kuweza kukagua magari yote ya abiria na mizigo ili kabla ya kushuka mteremko huo kuwa na uhakika wa breck kama njia ya kuanza kuchukua hatua za kukabiliana na ajali mbaya katika mteremko huo.
MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA ILALA JERRY SILAA ARUDISHA FOMU ZA UVCCM - NEC.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa akirejesha fomu za
kugombea nafasi ya ujumbe wa UVCCM-NEC katibu wa UVCCM mkoani Mwanza.
Bw. Elias Mpanda, katika ofisi za CCM mkoani- Jijini Mwanza. Mstahiki
meya Manispaa ya Ilala Bw. Jerry Silaa anagombea nafasi ya ujumbe wa
UVCCM-NEC ngazi ya taifa.
Mstahiki meya aliweka wazi nia yake ya kutaka kuwawakilisha vema
vijana wa kitanzania kwenye UVCCM-NEC na aliwaasa vijana wengine
kushiriki kwenye mchakato huo na huku akisisitza kwamba yuko tayari
kufanya kazi kokote nchini kwa maslahi ya wananchi, vilevile meya
aliwaasa viongozi wote kuwajibika na kutimiza ahadi zao walizozitoa kwa
wananchi na kwa kuweka mbele maslahi ya taifa na sio yao binafsi
SBL Moshi wamuaga aliyekuwa mkurugenzi wao Richard Wells
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda
(katikati) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (kulia) na Mkurugenzi
aliyemaliza muda wake Richard Wells wakati wa tafrija maalum ya kumuaga
Wells iliyofanyika Kiwanda cha SBL mjini Moshi hivi karibuni.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda
(wapili kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (wapili kulia) na Mkurugenzi
aliyemaliza muda wake Richard Wells (kushoto) na Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda wakati wa tafrija maalum ya kumuaga
Wells iliyofanyika Kiwanda cha SBL mjini Moshi hivi karibuni.
Mama Tundu Pinda akipeana mkono na
Mkurugenzi Mtendaji wa SBL aliyemaliza muda wake, Richard Wells wakati
wa tafrija ya kumuaga iliyofanyika kiwanda cha SBL mjini Moshio hivi
karibuni.
Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi mpya wa SBL, Steven Gannon
Richard Wells (kushoto) akiwa
akitika vazi la jadi la jamii ya Wamasaa pamoja na Kisu jamii ya sime
alilokabidhiwa na Wafanyakazi wa SBL mjini Moshi wakati walipomuaga
rasmi baada ya kumaliza muda wake na kumkaribisha Mkurugenzi Mpya Steven
Gannon.
Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Bia Serengeti Mjini Moshi wakipiga picha na viongozi wao.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda
(wapili kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (kulia) na Mkurugenzi
aliyemaliza muda wake Richard Wells (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya
Moshi Dr. Msengi
Mkurugemzi wa Mawasiliano wa SBL,
Teddy Mapunda akitunzwa na Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji wa SBL,
Nandi Mwiyombela kwa kutoa burudani ya aina yake wakati wa tafrija hiyo
ya kumuga Richard Wells.
Vijana wa Kalunde Band wakiwa kazini kutoa burudani
Hapa kazi tu.....Mkurugemzi wa
Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapundana Mkurugenzi wa Masoko Epraim Mafuru
wakiimba wakati wa tafrija hiyo ya kumuaga Richard Wells.
Richard Wells akicheza mziki na Wafanyakazi wa Kiwanda cha SBL mjini Moshi wakati wa tafrija ya kumuaga.
Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa SBL, Steven Gannon akisakata rumba na wafanyakazi wa SBL Kiwanda cha Moshi.
Wafanyakazi wakiwa wanaendelea na
vitu vya hapa na pale wakati wa tafrija hiyo ya mkumuga Mkurugenzi
Mtendaji aliyemaliza muda wake Richard Wells mjini Moshi.
MWITHA THOMAS
ZINAZOSOMWA ZAIDI
-
Mtangazaji wa Clouds FM Ephraim Kibonde "MANENO HAYA KUTOKA MDAU WA BLOG YA JAMII FORUM KWENDA KWA KIBONDE!" Ephraimu kibonde hii ndiyo ...
-
Msanii wa Bongo fleva Roma Mkatoliki amepata ajali mbaya ya gari Morogoro road ambapo kwa mujibu wa djchoka.blogspot.com ni kwamb...
Kumbu Kumbu
BLOG MBALI MBALI
VYOMBO VYA HABARI
Copyright 2012 © mwitha. All Rights Reserved.