I know, my last post might have given some hope that I would show up here more frequently. I confess I even thought I would. However, there is no way I can let recent events go unchronicled. I will start with the biggest event... the one that made national (international?) news this past week.
Last Wednesday, April 27, our state was hit with a record-breaking
number of tornadoes. One AP story quotes statistics of 226 tornadoes in
one day and 334 deaths in the 24 hours between 8am that morning and 8am
Thursday morning. We also had many severe thunderstorms accompanying the
tornadoes, with hail and strong winds. The storms caused a 2hour school
delay in the morning for schools in our area; as tornadoes began to
form in surrounding areas, most schools wound up letting out early (my
children's school has a tornado shelter, so it did not; my kids spent
about an hour in the shelter).
Noah and I were out in the storm at one point (had an appointment that
we didn't know had been canceled due to the weather) and stopped at a
local fast food restaurant just moments after a tornado had been sighted
less than a mile away (unbeknownst to us). Only a minute or two after
we placed our order, we were ushered to the kitchen of the restaurant,
where we got to wait out the storm for 30-45 minutes. During that time,
there was an area-wide power outage; most of northern AL had its power
knocked out, including where we were sitting and here at home. We were
able to get home during a lull in the storm. Emily had gathered our
candles and flashlights, so we were not totally in the dark.
Brian was still at work in Decatur (tornadoes were at work near him as
well); the hospital was on emergency generator power. He wound up having
to stay thru the night and next day, as the hospital was taking in
storm victims from surrounding communities. Another regional hospital
south of here in Cullman had taken a hit from a tornado, so could not
provide care to victims.
To make a long story short.... we were without power from Wednesday
afternoon until sometime during the early morning hours of Monday.
Thursday morning dawned sunny and beautiful. We had absolutely gorgeous
weather, temperate and clear for the remaining days. It wasn't until
late last night that another set of thunderstorms rolled in.
Our time without power was merely
an inconvenience, a slight one at that. Yes, we lost some food in the
refrigerator and freezer. That's really about it. The boys spent more
time outside than they ever do, getting to know the neighbor kids more,
riding bikes, hanging out... We played board games by candle- and
flashlight. Halle and I cut up magazines and made collages together.
(Definitely therapeutic.... I think we'll be doing more when our
magazine stash is built back up!). On Sunday afternoon, Brian and the
boys accompanied a group from church to help clean up a home that had
been hit by one of the tornadoes. The following newsclip includes a
short interview with Joel, and you can catch glimpses of Brian (bald guy
in maroon shirt) and Noah (tall kid in light blue shirt and basketball
shorts with backwards baseball cap).
KUKAMATWA KWA PONDA KOVA AORODHESHA TUHUMA DHIDIYAKE!
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalu ya Dar es Salam Suleimani Kova
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kukamatwa
kwa Sheikh Ponda Issa Ponda jana usiku baada ya kuweka mtego kwenye
eneo ambalo kwa mujibu wa kova ni mafichoyake na alipelekwa na pikipiki.
Katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh
Ponda Issa Ponda, wakti akiwahutubiwa waisilamu kwenye maandamano ya
hivi karibuni kupinga filamu iliotengenezwa marekani ya kukashifu mtume
kwenye viwanja vya Kidongo Chekundu.
KIONGOZI wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu nchini Sheikh Ponda Issa
Ponda ametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi jana usiku ambapo kwa mujibu wa
Kamanda Kova wamemkamata wakati akienda kwenye mafichoyake muda mfupi
tu baada ya kushushwa kwenye pikipiki kwenyeeneo la Chang'ombe jijini
Dar es Salaam.
Mbali na kukamatwa Kiongozi huyo pia watu wengine 38 wamekamatwa majira
ya saa 4:00 usiku baada ya kufanya operesheni maalum. Watu hao
wanakamatwa kwa madaikuwa ni wafuasi wa sheikh Ponda aliongoza kundi
hilo kuvamia kiwanja No.311/3/4BLOCK "T" eneo la Chang'ombe Manispaa ya
Temeke.
Kwenye Taarifa ya Kova kumeelezwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za
kusababisha vurugu na vitisho,
Sambamba na hilo Ponda na wafuasi wake anatuhumiwa pia kinume cha sheria
walisababisha kuvunjwa kwa makanisa zaidi ya manane siku ya 12/10/2012.
TAARIFA YA UCHUNGUZI WA KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI
WA CHANNEL TEN BW. DAUD MWANGOSI
1.0 UTANGULIZI
Mnamo tarehe 03 Septemba mwaka 2012, Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi (MB) aliteua Kamati ya watu watano
kufanya uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwandishi wa habari wa kituo cha
televisheni cha Channel Ten, marehemu Daud Mwangosi, kilichotokea tarehe
02 Septemba 2012, katika Kijiji cha Nyololo,Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa
Iringa. Kituo cha kazi cha marehemu Daud Mwangosi kilikuwa mkoa wa Iringa
ambapo pia alikuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa
Iringa (IPC).
Wajumbe wa Kamati hiyo ni:
Jaji (Mst.) Steven Ihema – Mwenyekiti
Bibi Pili Mtambalike – Mjumbe
Kanali (Dkt. Eng) Wema Wilson Wekwe – Mjumbe
Bwana Theophil Makunga – Mjumbe
Naibu Kamishna wa Polisi Issaya Juma. Mngulu – Katibu
Sekretarieti ya Kamati ni:
Bi. Edith T. Assenga – Wizara ya Mambo ya Ndani
Bwana Nasoro H. Msumi – Wizara ya Mambo ya Ndani
2.0 HADIDU ZA REJEA
Kamati ilipewa Hadidu za rejea zifuatazo:
- Uhalali wa mkusanyiko ulioitishwa na CHADEMA eneo la
Nyololo,Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa tarehe 02 Septemba, 2012 na kuwepo
kwa uvunjifu wa amani.
- Kama yalikuwepo makubaliano au maelekezo kuhusu mikutano ya
hadhara au maandamano nchini katika kipindi cha Sensa.
-Mazingira yaliyosababisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu
iliyosababisha kifo cha Marehemu Daud Mwangosi na wengine kuumizwa, na uwiano
wa nguvu hiyo na tukio.
-Madai ya kuwepo uhasama kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa
Habari Mkoa wa Iringa na chanzo cha uhasama huo. Aidha kuna madai ya kuwepo kwa
orodha ya waandishi watatu (3) ambao Jeshi la Polisi limepanga kuwashughulikia.
-Uwepo wa Sheria, Kanuni au Taratibu zinazotoa uwezo kwa Jeshi la
Polisi kuzuia mikusanyiko inayoitishwa na Vyama vya Siasa na Mamlaka ya Rufaa
endapo vyama hivyo havitaridhika na amri hizo.
-Hali ya Mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa
nchini katika Utendaji kazi wao na Utii wa Sheria.
3.0 MUDA WA UCHUNGUZI
Kamati ilipewa muda wa siku 19 kuanzia tarehe 11 Septemba 2012 iwe
imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha Ripoti yake ifikapo tarehe 02 Oktoba
2012.
4.0 NJIA ZILIZOTUMIKA KUFANYA UCHUNGUZI:
4.1 Mahojiano na watu mbalimbali waliokuwepo kwenye tukio.
4.2 Kupitia nyaraka na vielelezo mbalimbali.
4.3 Kutembelea eneo la tukio.
4.4 Majadiliano na vikundi mbalimbali (viongozi wa dini ngazi ya
kijiji na wilaya hadi ya mkoa; viongozi wa vyama vya siasa kwenye ngazi ya
kijiji, wilaya, mkoa na Taifa, viongozi wa serikali ngazi ya kijiji, wilaya,
mkoa, Taifa) na wanakijiji wa Nyololo.
5.0 UCHUNGUZI
Kamati ya Uchunguzi ilifanya mahojiano na watu mbalimbali ikiwa
pamoja na watendaji wa serikali hususan Kamati za Ulinzi na Usalama ngazi ya
wilaya Mufindi na mkoa wa Iringa viongozi wa Jeshi la Polisi viongozi wa vyama
vya Siasa, Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Waandishi wa Habari na wananchi wa
kawaida (ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa).
6.0. YALIYOJITOKEZA
Baada ya Kamati kukutana na makundi ya watu mbalimbali katika Mkoa
wa Iringa na Viongozi wa Vyama vya Siasa wa kitaifa jijini Dar es Salaam, mambo
kadhaa yalijitokeza na baadhi yao ni:
-Hofu ya kutoweka kwa amani miongoni mwa viongozi na wananchi hasa
katika mikutano na maandamano ya siasa ambayo yameanza kuota mizizi ya uvunjifu
wa amani na mengine kusababisha mauaji. Viongozi na wananchi wengi waliotoa
maoni yao mbele ya Kamati wameonyesha hofu kuwa hali hiyo isipodhibitiwa mapema
inaweza kulipeleka pabaya Taifa letu.
-Kuna walakini wa mahusiano kati ya waandishi wa habari na Jeshi
la Polisi mkoani Iringa.
-Uwepo wa utashi wa makusudi/dhati kwa viongozi wa vyama vyote vya
siasa kuweka mbele maslahi ya taifa badala ya maslahi ya vyama.
-Umuhimu wa Ushirikiano na mahusiano baina ya vyombo vya serikali,
vyama vya siasa, wanahabari na wananchi kwa ujumla badala kuonyeshana ubabe
ambao umetufikisha hapo.
- Haja ya kufanya mabadiliko ya kisheria katika mfumo wa usimamizi
na utendaji wa masuala ya siasa nchini
- Haja ya kuwa na mabadiliko ya kimfumo katika Jeshi la Polisi
badala ya ulioko sasa ambao kwa maoni ya baadhi ya watu waliozungumza na Kamati
ni wa kitaifa zaidi na kuacha serikali za mitaa bila ya wajibu wa kulinda
usalama wa raia na mali zao.
-Kwamba nguvu kubwa inatumika na vyombo vya dola/usalama dhidi ya
raia na hivyo kupunguza imani ya jamii kwa vyombo hivyo.
-Kupungua kwa maadili/uzalendo miongoni mwa Watanzania kuanzia
viongozi hadi wananchi hususan kwenye shughuli za kisiasa.
-Haja ya kusisitiza elimu ya uraia kwa jamii kuanzia kwa watoto
hadi kwa watu wazima hasa wakati huu wa mfumo wa vyama vingi ili kujenga umoja
wa kitaifa.
-Kuwepo kwa mikutano na maandamano ya vyama vya siasa yasiyokuwa
na kikomo.
-Muonekano wa Jeshi la Polisi mbele ya jamii.
7.0. MATOKEO YA UCHUNGUZI KUTOKANA NA HADIDU ZA REJEA
7.1 Kuhusu “Uhalali wa mkusanyiko ulioitishwa na CHADEMA eneo la
Nyololo, Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa tarehe 02 Septemba 2012 na kuwepo
uvunjifu wa amani”, uchunguzi wa Kamati umebaini yafuatayo:
Tarehe 30 Agosti 2012 CHADEMA iliandika barua, Ofisi ya Mkuu wa
Polisi Wilaya ya Mufindi kutoa taarifa kuhusu ratiba ya mikutano ishirini na
sita (26) kwenye majimbo ya Mufindi Kusini na Kaskazini tarehe 02-03 Septemba
2012. Awali ratiba ya mikutano hiyo ilikubaliwa, lakini baadaye siku hiyo ya
tarehe 01 Septemba 2012 mikutano hiyo ilisitishwa kwa barua Kumb. Na
MFG/A.24/9/54 kutokana na kuongezwa siku za zoezi la Sensa ya watu na Makazi
hadi tarehe 08 Septemba 2012.
CHADEMA walikataa kusitisha ratiba ya mikutano hiyo kama
inavyothibitishwa na Justin Leornard Mpotwa Katibu wa Wilaya ya Mufindi kwa
barua yake Kumb. Na CDM/M4/002/Vol.01/2012 ya tarehe 01 Septemba 2012 kuwa “pia
tunaomba ieleweke bayana kwamba kisheria shughuli zetu hazina mwingiliano na
wala kuhusiana na program iliyoongezwa ya Sensa. Kwa barua hii tunakuarifu kuwa
mikutano tuliyokutaarifu kuifanya kuanzia kesho tarehe 02 septemba 2012
itaendelea kama ilivyopangwa – CHADEMA VEMA”.
Aidha kuwepo kwa zuio la mikutano ya Siasa ya CHADEMA Mkoani
Iringa wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linathibitishwa na Amri ya
Utendaji (Operation Order) ya Kamanda wa Polisi Mkoa (SACP Michael Kamuhanda)
ya tarehe 01 Septemba 2012. Amri ya Utendaji ambayo ni amri halali ilitolewa
ili “kuzuia shughuli za Siasa (mikutano na maandamano) kipindi cha zoezi la
kitaifa la Sensa kuanzia tarehe 25 Agosti 2012 hadi 08 Septemba 2012”. Uhalali
wa Amri/Zuio hili ulithibitishwa pia na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini
katika barua yake Kumb Na. DA. 112/ 123/ 01/ 34 ya tarehe 28/08/2010 na wakati
wa mahojiano na Kamati ya uchunguzi tarehe 22 Septemba 2012.
Licha ya zuio/amri hii Viongozi wa CHADEMA walikataa kutii amri
hiyo. Kutokana na taarifa hizi, Kamati ya Uchunguzi inathibitisha kwamba
hapakuwepo na uhalali wa mkusanyiko/mkutano ulioitishwa na CHADEMA eneo la
Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa tarehe 02 Septemba 2012. Kuhusu
kuwepo kwa uvunjifu wa amani Kijijini Nyololo tarehe 02 Septemba 2012 Kamati ya
Uchunguzi ilibaini mambo yafuatayo:
-Tukio la kuuawa kwa Daud Mwangosi jioni ya tarehe 02 Septemba
2012 lilitokea baada ya Operesheni ya Jeshi la Polisi kumalizika. Hii ni kwa
mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Mkuu wa Kikosi cha
Kutuliza Ghasia Mkoa wa Iringa na Joseph Senga Mpiga picha/Mwandishi Tanzania
Daima.
- Kitendo cha kutotii amri halali ya Kamanda wa Polisi kuagiza
wafuasi wa CHADEMA watawanyike kutoka kwenye eneo la ofisi ya Kata ya CHADEMA
ilikuwa chanzo cha vurugu.
Uamuzi wa CHADEMA kung’ang’ana kukusanyika isivyo halali eneo la
Nyololo ikizingatiwa kuwepo kwa ujumbe wa SMS kutoka kwa Dkt. Slaa, Katibu wa
CHADEMA uliosema, “IGP nasubiri simu yako. Wajulishe Polisi wako waandae risasi
za kutosha, mabomu ya kutosha. Mtakuwa na karamu ya mauaji na kisha
kusherehekea, mjiandae kwa kwenda mahakama ya Den Hague. Ni afadhali tufe
kuliko manyanyaso haya”. Dr. Slaa. : ujumbe huu ukiashiria umwagaji wa damu ni
ushaidi tosha kuwepo kwa uvunjifu wa amani. CHADEMA ndiyo Chanzo cha vurugu na
uvunjifu wa amani Kijijini Nyololo tarehe 02 Septemba 2012.
7.2 Kama yalikuwepo makubaliano kuhusu mikutano ya hadhara au
maandamano nchini katika kipindi cha Sensa. Katika kuzungumzia hoja hii
tukianzia na Uongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi
Taifa, Kamati ya Uchunguzi ilithibitisha kuwepo kwa maagizo ya kusimamisha
mikutano/maandamano ya Vyama vya Siasa wakati wa kipindi cha Sensa ya Watu na
Makazi yaliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, na kuongezwa muda wa
Sensa hadi tarehe 08 Septemba 2012 na Kamishna wa Sensa hapo tarehe 01 Septemba
2012.
Aidha hoja hii imethibitika kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini kwa barua yake yenye Kumb Na DA. 112/ 01/ 34 ya terehe 28 Agosti 2012
kwenda kwa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa akiwasihi kusimamisha shughuli
zote za mikutano na maandamano ya Vyama vyao kwa kipindi chote cha Sensa ya
Watu na Makazi. Aidha kwa mujibu wa Gazeti la Serikali Na 29 VOL 93 ya tarehe
20 Julai 2012, Mhe. Rais, JAKAYA MRISHO KIKWETE kwa mamlaka aliyopewa chini ya
kifungu namba 14 cha Sheria ya Takwimu sura 351 alielekeza kwamba Sensa ya Watu
na Makazi itafanyika kuanzia tarehe 26 mwezi wa nane, mpaka tarehe 08 mwezi wa
tisa mwaka 2012.
Kamishna wa Sensa aliratibu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi
kumalizika ifikapo tarehe 01 Septemba 2012. Hata hivyo kutokana na tathmini
aliyofanya, kazi hiyo ilikuwa imekamilika kwa asilimia 95%. Hivyo tarehe 01
Septemba 2012 alitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari kwamba ili kila mwananchi
apate nafasi ya kuhesabiwa watu watakaokuwa wamesalia ambao ni chini ya 5%
wanaombwa kutoa ushirikiano ili zoezi hili likamilike. Hivyo, wale wote mmoja
mmoja waliobakia wataendelea kuandikishwa hadi tarehe 08 Septemba 2012.
Kwa upande wake Inspekta Jenerali wa Polisi kwa ujumbe wa simu
Kumb Na S8.7/ 2/ A/ VOL XIV/ 59 ya tarehe 28/08/2012, pia simu yake Kumb Na
C.28/ B/ 44 ya terehe 01/ 09/ 2012 aliwaelekeza Makamanda wa Polisi wa Mikoa
kutoruhusu mikutano na maandamano wakati huu wa zoezi la Sensa ya Watu na
Makazi mpaka litakapokamilika tarehe 08 Septemba 2012.
Kimsingi Kamati ya uchunguzi imethibitisha kwamba maelekezo kwa
Vyama vya Siasa kutoendesha shughuli za mikutano ya hadhara au maandamano
yalitolewa kwa mujibu wa Sheria.
7.3 Mazingira yaliyosababisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu
iliyosababisha, kifo cha marehemu Daud Mwangosi na wengine kuumizwa, na uwiano
wa nguvu hiyo na tukio.
Hoja kuwa Polisi walitumia nguvu kubwa katika kudhibiti mkutano wa
CHADEMA iliungwa mkono na Viongozi wa Serikali ya Kijiji, Viongozi wa dini na
Viongozi wa siasa Kijijini Wilayani na Mkoani pamoja na Waandishi wa Habari.
Hata hivyo Kamati za Ulinzi na Usalama Wilaya na Mkoa na Viongozi wa Jeshi la
Polisi waliona nguvu hizo ni za mazingira ya hali ilivyokuwa.
Uchunguzi wa suala hili umebaini kwamba tarehe 02 Septemba 2012
muda wa saa 10 za jioni huko eneo la Sokoni, Kijiji cha Nyololo kulikuwepo na
mkutano usio halali ulioandaliwa na viongozi wa CHADEMA. Upo ukweli kwamba
uongozi wa Polisi ulitoa ilani kuamuru wafuasi wa CHADEMA waliokuwepo mkutanoni
hapo waondoke la sivyo nguvu itatumika. Walikaidi amri hiyo na ilipoagizwa
viongozi wakamatwe ndipo walianza kurusha mawe kwa Askari Polisi. Baadhi ya
Askari walijeruhiwa, akiwamo G 9934 PC Mgaka alivunjwa mkono wa kulia. Pia
kofia (helmet) tatu ziliharibiwa.
Kutokana na hali hiyo amri ya kupiga mabomu ya machozi na ya
kishindo ilitolewa, kwa mujibu wa Kifungu 77 hadi 79 cha Kanuni za Adhabu, Sura
ya 16 – R.E 2002. Operesheni hii ilimalizika baada ya kukamatwa viongozi na
wafuasi wa CHADEMA jumla yao saba.
Baada ya zoezi hilo kukamilika Askari Polisi walioshiriki kwenye
Operesheni waliamriwa kuingia katika magari tayari kwa kuondoka. Wakati Askari
wakipanda kwenye magari kishindo kikubwa kilitokea umbali wa zaidi ya mita 100
kutoka sehemu ambayo operesheni ilikuwa inafanyika na iligundulika kwamba
kishindo kile kimesababisha kifo cha Mwandishi wa Habari Daud Mwangosi.
Upelelezi wa awali pamoja na picha za mnato unaonyesha kwamba
marehemu alikuwa amemkumbatia Mkuu wa Polisi Kituo cha Mafinga ASP Assel
Mwampamba na huku akiwa amezungukwa na Askari Polisi wasiopungua sita ambao
licha ya kumzunguka marehemu Daud Mwangosi kuna madai yaliyotolewa na mwandishi
wa Habari Joseph Senga kwamba, Askari Polisi hao walikuwa wanamshambulia
marehemu kwa kumpiga, ndipo askari mmoja aliyetambuliwa kuwa ni G 2573 PC
Pasificus Cleophace Simon alifyatua Bomu la kishindo na kusababisha kifo cha
Daud Mwangosi.
Tukio hili linaweza kugawanyika katika sehemu mbili: sehemu ya
kwanza ni wileamapamebas(mni ya kutawanya watu na ya pili ni ile ya mauaji ya
Daud Picha Namba 15: Askari Polisi wakimpiga Marehemu Daud Mwangosi, huku OCS M
wenye kifimbo) akijaribu kuwazuia. Mwangosi. Katika tukio la kwanza idadi ya
Askari walioshiriki ni Sekisheni Tukio hili linaweza kugawanyika katika sehemu
mbili: sehemu ya kwanza ni lile ya Operesheni ya kutawanya watu na ya pili ni
ile ya mauaji ya Daud Mwangosi.
Katika tukio la kwanza idadi ya Askari walioshiriki ni
Sekisheni tatu ambapo ni askari wasiozidi thelathini. Kwa maelezo yaliyotolewa
na Mwandishi wa Habari mbele ya Kamati, Bw Joseph Senga anaeleza kuwa watu
walishatawanyika na hali kutulia mara baada ya Operesheni hii kukamilika na
Polisi kujiandaa kuondoka kwenye eneo la tukio. Tukio la mauaji ya Daud
Mwangosi lilisababishwa na kupigwa bomu la kishindo.
Maswali ya kujiuliza katika tukio la mauaji ni Je, kulikuwepo na
uwiano unaolingana na tukio hili?, Je Palikuwa na uhalali wa kutumia Bomu la
kishindo?, na Je, utumiaji wa Bomu hilo ulikuwa na umuhimu?
Kulingana na tukio lenyewe majibu ya maswali hayo ni kama
ifuatavyo:
-Hapakuwa na uwiano wa Bomu na tukio la mauaji, kwa vile utaratibu
wa matumizi ya bomu hilo unaelekeza kulenga juu usawa wa nyuzi 45 na umbali
mita 80 mpaka mita 100.
-Hapakuwa na uhalali wa kutumia Bomu la Kishindo kwani lengo la
ulipuaji wake ni ili watu waogope na kukimbia.
- Hapakuwepo umuhimu wa kutumia Bomu la Kishindo kwa sababu hata
ingekuwa ukamataji tayari Askari Polisi wapatao sita walikuwepo eneo la tukio.
Kwa misingi hiyo Kamati imeona kwamba nguvu iliyotumika mwanzo
hadi kumaliza Operesheni haikuwa kubwa. Kuhusu tukio la kuuawa Bw. Daud
Mwangosi na kuumizwa baadhi ya Askari Polisi halikustahili kabisa.
7.4 Madai ya kuwepo uhasama kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi
wa Mkoa wa Iringa na chanzo cha uhasama huo. Aidha madai ya kuwepo kwa orodha
ya waandishi watatu (3) ambao Jeshi la Polisi limepanga kuwashughulikia.
Katika kupata ukweli wa jambo hili, Kamati ilikutana na wanachama
wa Klabu ya Waandishi wa Habari Iringa na pia iliwahoji Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa, Nyigesa Ramadhani
Wankyo na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoani Iringa Said Abdallah Mnunka.
Pia, wakati Kamati inakutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa, ilileta suala la mahusiano kati ya Polisi na waandishi wa habari na
watendaji wakuu wa serikali wa mkoa wa Iringa.
Katika mkutano na waandishi wa habari, ilionekana kuwa katika
thathmini yao uhusiano kati yao na Polisi hapo mkoani ni mbaya sana. Walieleza
matukio kadhaa ya kunyanyaswa waandishi wa habari wakati wapo kazini, ikiwamo
kupigwa, kutishiwa kuharibiwa na kuharibiwa vifaa vyao vya kazi na hata
kutishiwa maisha ili wasiripoti mambo ambayo Polisi wana maslahi nayo.
Kwa mfano, mwandishi wa habari wa Star TV, Oliver Moto alieleza
Kamati kuwa: “Waandishi wa habari hawana mahusiano mazuri na Jeshi la Polisi,
na hata wanapofika ofisi za Polisi huwa hawapewi ushirikiano. Kutokana na uhusiano
mbaya wanahabari walifanya maandamano tarehe 06 Machi 2012 kupinga unyanyasaji
wanaofanyiwa na Jeshi la Polisi hapa Iringa”.
Mwandishi mwingine wa habari Zulfa Shomari ambaye anaandikia
gazeti la Mwananchi alieleza kuwa kuna matukio kadhaa ambayo Polisi wamewazuia
waandishi kufanya kazi zao mojawapo ni lile ambalo Polisi walikataza kupigwa
picha tukio la kukamatwa kwa pembe za ndovu.
Kamati pia iielezwa na mwandishi wa habari wa ITV, Bw. Laurian
Mkumbata mkasa wa kuvunjwa kamera yake na OCD Iringa kwenye tukio moja. Ilibidi
OCD alipe kamera hiyo kwa maagizo ya RPC.
Pia walisema kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa hivi sasa ana
mawasiliano duni sana na waandishi wa habari na juhudi za wengi wao kumfuata
ili athibitishe tukio zimekuwa zikishindwa kwani ameweka maagizo getini kuwa
mtu yeyote ambae anataka kumuona ni lazima aeleze anataka kumuona kwa sababu
gani ndipo aruhusiwe kuingia. Kwa sababu hii waandishi wa habari wengi wamekata
mguu kwenda ofisini kwake.
Mwandishi mmoja wa Ebony FM Bw. Raymond Francis, aliiambia Kamati
kuwa yeye binafsi alitishiwa kuuawa na baada ya kuandaa kipindi kuhusiana na
watu wanaoshukiwa kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevya ambao
wanahusiana na baadhi ya Polisi wasio waadilifu.
Mwandishi wa Habari Greyson Mgoi wa gazeti la Kwanza Jamii
aliiambia Kamati kuna tukio la kuanguka kwa lori la mafuta eneo la Ifunda
karibu na Mafinga ambapo waliwakuta wananchi na polisi wakichota mafuta kutoka
kwenye hilo gari.
Alisema kuwa waliamua kupiga picha tukio hilo lakini Polisi waliwakamata
na kuwalazimisha wafute hizo picha walizopiga. Kwa kuogopa shari walikubali
kuzifuta na wakaruhusiwa kuendelea na safari yao.
Waandishi wa Habari hata hivyo walibainisha kuwa uhusiano wao na
Polisi hapo mkoani ulikuwa mzuri sana kipindi cha uongozi wa RPC Advocate
Nyombi. Walisema kuwa wakati wa RPC Nyombi, alikuwa na utaratibu wa kukutana na
waandishi wa habari na pia alikuwa anafikiwa na waandishi wa habari kwa urahisi
kwa simu au ofisini kwake. Walisema lakini ulianza kuharibika alipohama na
nafasi yake kuchukuliwa na RPC Mangara na kuwa mbaya zaidi alipokuja Kamuhanda.
Walidai kuwa Polisi wa Iringa si waadilifu na wamekuwa wakijiona kama miungu
watu.
Waandishi walieleza Kamati, kitu kilichowaudhi sana ni yale majibu
yaliyotolewa na RPC baada ya mauaji ya Daud Mwangosi ambayo yalionekana
yalikuwa ni ya kupanga ili ukweli usijulikane. Walisema kama si picha
zilizotolewa na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye tukio, hawadhani kama
umma wa Watanzania wangepata ukweli wa tukio hilo.
Walisema tarehe 06 Machi 2012, walifanya maandamano ili kupinga
manyanyaso ya Polisi wa mkoani Iringa yaliyopokelewa na Mkuu wa Mkoa. Waandishi
wa Habari mkoani Iringa pia walionyesha masikitiko yao kuwa tangu kutokee kwa
mauji ya Daud Mwangosi, hawajapokea pole kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na watendaji
wake wa juu hata kama ni ya “kinafiki”.
Kwa upande wa pili, yaani Jeshi la Polisi, Kamati ilipata taswira
tofauti. RPC Kamuhanda alisema kuwa yeye anaona mahusiano ya Polisi na
waandishi wa habari kwa ujumla ni mzuri na yeye binafsi amekuwa akikutana na
waandishi wa habari takriban kila siku asubuhi saa nne kuwapa habari. Pia
aliiambia Kamati kuwa waandishi wa habari walishiriki kikamilifu katika
kuripoti michuano ya mpira ya Kikombe cha Kamuhanda yaliyofanyika mjini Iringa.
Msimamo huo pia ulichukuliwa na viongozi wa juu wa kiutawala
akiwemo Mkuu wa Mkoa Dkt. Christine Ishengoma, Katibu Tawala wa Mkoa Bibi
Getrude Mpaka ambao walisema kuwa hapakuwa na uhasama wowote kati ya Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa na Waandishi wa Habari. Wote wawili walisema kuwa walimfahamu
marehemu Daud Mwangosi na aliteuliwa katika kamati kadhaa za kimkoa ikiwa ni
pamoja na ile ya kuandaa Sensa ya Watu na Makazi Mkoani, Kamati ya Masuala ya
Katiba ya Mkoa na Kamati ya Kukuza Utalii ya Mkoa.
Kuhusiana na hisia kuwa Mkuu wa Mkoa na watendaji wake
hawakujumuika na waandishi katika msiba wa Daud Mwangosi, Dkt. Ishengoma
alisema si kweli hawajatoa rambirambi zao kwa kifo cha Mwangosi lakini alitoa
pole kwa waandishi wakati ameenda na IGP Mwema kijijini Nyololo na pia kupitia
radio katika kipindi kilichotayarishwa na mwandishi wa habari Francis Godwin.
Baada ya kuongea na pande hizo mbili, Kamati imebaini kwamba kuna
walakini wa mahusiano kati ya waandishi wa habari na baadhi ya askari polisi
mkoani Iringa. Kuhusu madai ya kuwepo kwa orodha ya waandishi watatu (3) ambao
jeshi la polisi limepanga kuwashughulikia.
Kwenye tukio la Nyololo ambapo mwandishi wa habari Daud Mwangosi
aliuawa, mwandishi wa habari mwengine Godfrey Mushi alipigwa na Polisi na
inasemekana kujeruhiwa vibaya na baadaye kukamatwa na Polisi.
Kwa mujibu wa Joseph Senga mpiga picha/mwandishi wa habari wa
gazeti la Tanzania Daima ambaye alikuwepo kwenye tukio na kupiga picha,
alimuona marehemu akipita nyuma ya gari moja la Polisi ambalo lilikuwa na baadhi
ya wanachama wa CHADEMA. Punde tu alimwona mtu amezungurukwa na askari akipigwa
lakini hakujua ni nani na yeye aliendelea kupiga picha tukio hilo mpaka nae
alipokamatwa na Polisi watatu ambao walimwuliza kama nae anataka aende kuungana
na mtu anayepigwa pale.
Senga alisema wakati kipigo kinaendelea, kuna askari mmoja mwenye
nyota tatu (OCS Mwampamba) aliteremka kutoka kwenye gari na kwenda pale ambapo
Yule mtu aliyekuwa anapigwa huku akiwaambia “mwachieni, mwachieni, namfahamu
mimi huyo ni mwandishi wa habari!”
Senga alisema mara alisikia kishindo kikubwa na wale askari ambao
walikuwa wanamshikilia walikimbia ndipo yeye akaendelea kupiga picha sasa za
marehemu Daud Mwangosi ambaye alikuwa amekwisha sambaratishwa na bomu. Alieleza
kuwa alimsikia yule askari ambaye alikuja kumsaidia marehemu Mwangosi akisema
“afande wameniuwa”, “afande wameniuwa”, akimwambia RPC ambaye alikuwa karibu
nae kwani nae aliumizwa vibaya katika mlipuko huo. Senga aliiambia Kamati wale
wote ambao walikuwa wame mzunguka marehemu kama wanavyoonekana kwenye picha
alizopiga walikuwepo wakati anapigwa.
Maelezo ya Bw. Senga yanatofautiana sana na yale yaliyotolewa na
RPC na OC FFU kuwa Marehemu alimvamia OCS Mwampamba na kuwa wale askari huenda
walidhania kuwa mkubwa wao alikuwa amevamiwa ndipo walipoamua kwenda kumsaidia.
OCS Mwampamba mwenyewe wakati akihojiwa na Kamati ilipokuwa Mafinga alisema
hakumbuki kitu.
Hata hivyo, kwa maelezo ya Bw. Senga, ambayo yanakubaliana na yale
ya RPC na OC-FFU, kitendo cha kupigwa na mauaji ya marehemu Daud Mwangosi
kilitokea baada ya kuisha ile operesheni ya kusambaratisha mkutano wa CHADEMA
na hapakuwa na mabishano yeyote au purukushani iliyotokea kabla ya
marehemu kuzungukwa na kuanza kupigwa.
Kwa minajili hii basi Kamati imeshindwa kubaini baada ya kumalizika
operesheni na askari Polisi kuanza kuondoka, kwa nini Mwangosi alishambuliwa
kwa kipigo kabla ya kulipuliwa na bomu la kishindo?
Kwa nini kuna maelezo yanayokinzana kati ya Bw. Senga ambaye
alikuwa karibu sana na tukio na yale ya RPC na OC-FFU ambao katika maelezo yao
kwa Kamati walisema kuwa wao walikuwa mbali kidogo na tukio kwa hiyo hawakuweza
kuona kwa dhahiri kilichotokea. Maelezeo ambayo yalirudiwa na viongozi wa juu
wa Polisi ikiwa ni pamoja na Kamishna wa Upelelezi (DCI) Robert Manumba na Inspekta
Jenerali wa Polisi, Said Mwema katika mahojiano na Kamati.
Uchunguzi wa Kamati haukuweza kupata ushahidi wa kubainisha kama
kupigwa kwa waandishi hao kulitokana na njama yeyote ya Polisi kuwashughulikia
au ilitokea kwenye purukushani ya vurugu zilizotokea baada ya FFU kuamriwa
kutawanya wanachama wa CHADEMA.
Pia Kamati haikupata ushahidi wowote wa kuonyesha kuwa mauaji ya
Daud Mwangosi yalikuwa ni ya kupangwa. Kutokana na maelezo ya hapo juu, Kamati
inapendekeza yafuatayo:-
-Taasisi za habari zinazosimamia maadili na weledi wa vyombo vya
habari, hususan Baraza la Habari Tanzania na Jukwaa la Wahariri wafanye
utaratibu unaostahiki za upatanishi kati ya waandishi wa habari, Jeshi la
Polisi na uongozi wa mkoa wa Iringa. Hii itasaidia kurejesha uhusiano mzuri
kati ya vyombo hivyo muhimu katika mkoa;
-Waandishi wa habari wapewe mafunzo ya jinsi ya kuripoti matukio
ya hatari/ghasia;
-Waandishi wa habari wavae vivazi maalum vya kuwatambulisha wakiwa
katika matukio hasa kwenye maeneo hatarishi;
- Waandishi wa habari wafanye kazi kwa weledi, uadilifu, uwazi na
wasijibainishe na vyama vya siasa;
- Polisi ambao walihusika katika kumpiga marehemu Daud Mwangosi
kabla hajauawa wachukuliwe hatua stahiki za kisheria;
- Kamati ya Ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa
Habari iliyoanzishwa mwaka 2008 ifufuliwe. Na kamati hizo ziteremke hadi kwenye
ngazi ya mkoa kama ilivyokuwa awali.
- Viongozi wa polisi wanapotoa taarifa za tukio, ziwe zimefanyiwa
utafiti wa kina ili zisipotoshe jamii.
7.5 Uwepo wa Sheria, Kanuni au Taratibu zinazotoa uwezo kwa Jeshi
la Polisi kuzuia mikusanyiko inayoitishwa na Vyama vya Siasa na Mamlaka ya
Rufaa ambapo Vyama hivyo havitaridhika na amri hiyo.
Sheria Namba 5 ya 1992 kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 7 ya
2009 inaratibu mahusiano ya kiutendaji kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya
Siasa. Kwa mujibu wa Sheria hii Jeshi la Polisi limepewa madaraka ya kutoa zuio
kwa maandishi na kuweka bayana sababu za kuzuia mikutano au maandamano. Zuio
aina hii ni halali kwa mujibu wa Sheria na ni sherti Chama cha Siasa kiheshimu
na kutii. Fungu la 11 vifungu vidogo Na 1, 4, 5, 6, 7 na 8 ya Sheria ya Vyama
vya Siasa likisomwa pamoja na mafungu Namba 43, 44, 45 na 46 ya Sheria ya Jeshi
la Polisi na Auxiliary Forces Act Sura 322 vitatumika kusimamia uendeshaji
mikutano ya Vyama vya Siasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pamoja na kwamba Vyama vya Siasa vinatakiwa kutoa taarifa na
siyo kuomba idhini, Jeshi la Polisi limepewa uwezo na madaraka juu ya mikutano
hiyo kuhusu kuzuia au kuruhusu na au kutoa maelekezo stahiki, kama vile
kupendekeza, na kushauri eneo mbadala na tarehe tofauti ya kufanya
mikutano/maandamano.
Aidha kutotii amri/zuio ya Jeshi la Polisi ni kosa la Jinai kwa
mujibu wa Fungu la 74 la Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura 16 RE.
Vilevile kwa mujibu wa Fungu la 43 (6) ya Sheria ya Jeshi la
Polisi na Auxiliary Forces Act, Waziri wa Mambo ya Ndani ndiye Mamlaka ya Rufaa
dhidi ya amri/zuio linatolewa na Jeshi la Polisi.
Pamoja na kuwepo kwa Sheria hizi mbili bado kuna mapungufu katika
uendeshaji na usimamizi wa shughuli za Siasa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Kwa mfano pamoja na madaraka aliyonayo Msajili wa Vyama vya Siasa ya kukifuta
Chama cha Siasa kwenye rejesta ya usajili kwa mujibu wa Fungu la 19 na 20 ya
Sheria ya Vyama vya Siasa, kusimamisha utoaji wa ruzuku na matumizi yake,
uratibu wa shughuli za vyama hivyo hauko mikononi mwake.
Wadau wanashauri umuhimu wa kuimarisha uhusiano katika shughuli za
utendaji kati ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi ili
kudumisha utulivu na amani na utii wa sheria bila shuruti kwa upande mmoja na
kukuza mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa kwa upande mwingine.
7.6 Hali ya mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa
nchini katika utendaji kazi wao na Utii wa Sheria.
Kamati ya Uchunguzi wa Kifo cha Mwandishi wa Habari wa Channel
Ten, Daud Mwangosi katika kupata majibu kwa hadidu hii ya rejea, ilizungumza na
viongozi wa vyama vya siasa kutoka ngazi za Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya
Mufindi, Mkoa wa Iringa na Viongozi wa kitaifa jijini Dar es Salaam na viongozi
wa dini kutoka ngazi za Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi na Mkoa wa
Iringa.
Kwa ujumla, kila kiongozi wa chama cha siasa wa ngazi zote ambaye
Kamati imezungumza naye kuhusu hadidu hii ya rejea, ameelezea umuhimu wa Jeshi
la Polisi katika kulinda usalama wa raia na mali zao na wangependa jeshi hilo
liachwe huru katika kutekeleza majukumu yake bila ya kuingiliwa na wanasiasa
ili lifanye kazi zake kwa weledi na uadilifu.
Hata hivyo taswira iliyojitokeza ni kwamba kuna mgawanyiko wa
mtizamo kuhusu jinsi Jeshi la Polisi linavyoshughulikia mikutano/maandamano ya
Vyama vya Siasa.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wanaamini kuwa Jeshi la
Polisi linakipendelea Chama cha Mapinduzi na kubinya vyama vya upinzani, huku
viongozi wa CCM kutoka ngazi ya kijiji hadi Taifa wakilisifia Jeshi hilo kuwa
linafanya kazi yake vizuri na kwa weledi mkubwa.
Mgawanyiko wa taswira kuhusu madai kuwa Jeshi la Polisi
kuipendelea CCM hauko tu kati ya vyama vya upinzani na CCM bali pia kwa
viongozi wa dini kuanzia ngazi za kijiji, wilaya hadi mkoani Iringa kwa maelezo
kuwa hawajasikia hata siku moja mtu anauawa na Polisi kwenye mkutano wa CCM.
Mwandishi mmoja alitoa udadisi wake kuwa huwa wanapata shida sana kuandika
habari za mikutano ya CHADEMA kutokana na jinsi Polisi wanavyojipanga kwenye
mikutano ya chama hicho.
Kudhihirisha umuhimu wa Jeshi la Polisi katika jamii, hata wale
wanaolituhumu kuwa linakipendelea CCM, katika kutoa maoni yao kuhusu hatua za
kuchukuliwa askari wanaoharibu sifa ya Jeshi hilo, wanapendekeza kuwa askari
wahusika wachukuliwe hatua na kuomba Jeshi hilo liendeshwe kwa weledi hasa
inapotokea askari akalazimika kutumia silaha kukabiliana na fujo isifikie kuua.
Kwa mfano, Mchungaji Peter Katanga wa Revival Baptist Church,
alishauri chombo cha Polisi kisitumike kufanya mauaji, au kisitumike na mtu,
watu, au kikundi chochote kufanya matendo yasiyo mazuri kwa jamii kwa sababu
chombo hicho kipo kwa ajili ya kulinda usalama wa raia wote na mali zao.
Viongozi wa siasa wengine bila kujali itikadi zao, wameonekana
kukerwa sana na tabia ya watu kuuawa wakati Jeshi la Polisi linatuliza ghasia
na hii ikiachiwa iendelee inaweza kuleta uvunjifu wa amani katika nchi. Kwa
mfano, Mchungaji wa Kanisa la EFATA Nyololo, Mkombozi Kiliwa alishauri Polisi
watumie njia zinazofaa kukabiliana na wanaovunja sheria na si kuua.
Pia Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyololo, Obby Kimbale, alielezea
kutokukubaliana kwake na kitendo cha mauaji ya Daud Mwangosi, alipendekeza
elimu ya uraia itolewe kwa jamii nzima vikiwemo vyombo vya dola, viongozi wa
serikali, wanasiasa na wananchi kwa ujumla wao ili kila mtu kwa nafasi yake
akaelewa namna ya kutimiza wajibu wake ndani ya mfumo wa demokrasia ya vyama
vingi.
Kwa upande mwingine, wengi waliotoa maoni yao juu ya mahusiano ya
Polisi na vyama vya siasa, pamoja na kulaumu Jeshi la Polisi kutumia nguvu
kubwa katika kukabiliana na wafuasi wa CHADEMA, pia waliwalaumu viongozi wa
chama hicho, kwa kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi hatimaye kusababisha Polisi
kutumia nguvu kiasi hicho.
Kitendo cha kuuawa kwa Mwandishi wa Habari, Daud Mwangosi na tabia
ya kutokea mauaji katika mikutano ya CHADEMA kimeonekana kuwakera viongozi
wengi wa vyama vya siasa kwani wanaamini kuwa Polisi huwa wanatumia nguvu kubwa
kupita kiasi ‘wanapotuliza ghasia’ katika mikutano ya CHADEMA.
Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa, Zakaria Mwansasu alielezea sababu
ya matukio ya namna hii kuwa ni kutokana na mmomonyoko aliouita mkubwa wa
maadili hasa katika vyama vya siasa na akashauri viongozi wa vyama vya siasa
wakapewa elimu ya uraia.
Maoni mengi ya viongozi wa vyama vya siasa yamejikita zaidi katika
hofu ya nchi kuingia kwenye vurugu na kutoka kwenye kisiwa cha amani na hivyo
kutoa uashauri kwa viongozi wa vyama vya siasa na Jeshi la Polisi kuweka mbele
maslahi ya taifa.
Mchungaji Yokonia Koko wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), alielezea ukosefu wa maadili kwa baadhi ya askari Polisi kuwa umetokana
na jeshi hilo kuajiri vijana ambao hawana maadili na kwamba watuhumiwa wa
mauaji kwenye matukio yanayolihusisha Jeshi la Polisi wakati wa kuzuia fujo
katika mikutano/maandamano ya vyama vya siasa wachukuliwe hatua kali ili iwe
fundisho kwa askari wengine.
Kasi ya CHADEMA kuendesha mikutano katika sehemu mbalimbali nchini
kwa ajili ya kujiimarisha kichama, imepokewa kwa hisia tofauti na vyama vingine
vya siasa. Wakati kuna makundi ya watu katika jamii wakidhani kuwa hiyo ni haki
yao kama chama cha siasa kinachotaka kukua na kukubalika kisiasa, wengine
wanaiona mikutano hiyo ya hadhara ya CHADEMA kama ni kuwapunguzia muda wa
kufanya shughuli zao za maendeleo hasa baada ya kipindi cha uchaguzi
kumalizika.
Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama, alishauri kufanyiwa marekebisho
kwenye sheria ya Vyama vya Siasa Namba 5 ya mwaka 1992 itakayoweka wazi
shughuli za vyama vya siasa baada ya Uchaguzi Mkuu. Alisisitiza kuwa shughuli
za siasa baada ya Uchaguzi Mkuu zihamie bungeni kwa wanasiasa kuhoji mipango ya
maendeleo ya serikali na matumizi ya rasilimali za nchi na wananchi waachwe
wachape kazi zao za maendeleo.
Kuhusu Jeshi la Polisi, Mukama alisema mfumo uliopo wa Jeshi hilo
unalifanya lionekane la kitaifa zaidi na kushauri libadilishwe kimuundo ili
liweze kutandaa hadi serikali za mitaa kuongeza nguvu katika mpango wa ulinzi
shirikishi ulioanzishwa na Jeshi hilo.
Mwanasiasa John Shibuda alizungumzia mahusiano kati ya vyama vya
siasa na Jeshi la Polisi kwa kutoa lawama kwa vyama vya siasa kuwa havitoi
malezi kwa wanachama wake ambayo yatawafanya wawe waadilifu, wazalendo,
waaminifu na watiifu wa sheria.
Alisema vyama vya siasa havina mfumo wa kujihakiki, kujikosoa na
kujiwajibisha na akapendekeza kuanzishwa kwa mfumo huo kisheria ambao
utawajibisha vyama vya siasa kwa matendo ya viongozi au wanachama wao.
Shibuda alifafanua kwamba sheria anayopendekeza iwe na nguvu ya
kutoa adhabu kwa chama cha siasa na kwa kiongozi au mwanachama ambaye
atathibitika kuwa ndiyo chanzo cha uvunjifu wa amani.
Kuhusu Jeshi la Polisi mwanasiasa huyo alipendekeza kufanyike kwa
marekebisho ya utendaji ili wakuu wa wilaya na mikoa waondolewe nguvu za
kiutawala ambazo huwafanya wakati mwingine kutoa maagizo ya kisiasa kwa Jeshi
la Polisi na hatimaye kulifanya Jeshi hilo lionekane linatekeleza maslahi ya
wanasiasa badala ya kuwa chombo cha kulinda amani.
Kwa ujumla Kamati kutokana na maelezo mbalimbali ya Viongozi wa
Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi, imeona kuwa kuna mahusiano hafifu kati ya
baadhi ya Vyama vya Siasa na Jeshi la Polisi.
Kwa kuwa taasisi zote hizi ni wadau muhimu wa amani na utulivu
nchini, Kamati inapendekeza:
-Kuwe na jukwaa la mazungumzo ya mara kwa mara kati ya Jeshi la
Polisi na Vyama vya Siasa ili kila upande ujue wajibu wake na wa taasisi
nyingine katika kudumisha amani ya nchi na utamaduni wa kuheshimu sheria
zilizopo na kupunguza migongano.
-Kuhusu madai kwamba mauaji yanayotokea nchini yaundiwe Tume,
Kamati imeona kuwa zipo sheria zinazotoa mamlaka ya kutafiti au kuchunguza
endapo kuna mashaka ya kifo hicho.
-Muundo uliopo wa Jeshi la Polisi uangaliwe upya kisheria ili
kuziba mianya inayotoa nafasi kwa wanasiasa kulitumia Jeshi hilo kwa manufaa ya
kisiasa.
-Nafasi za Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa kiutendaji ziangaliwe
upya ili zisitumike na mhusika kwa ajili ya manufaa ya kisiasa.
-Kwa kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuwa ndiye mlinzi wa usalama
wa raia na mali zao, siasa za ubabe kwa vyama vya siasa ziepukwe kwa kuwa
zinaleta msuguano usio wa lazima na Jeshi la Polisi
8.0. MAONI NA MAPENDEKEZO:
Kutokana na uchunguzi uliofanyika kupitia mahojiano na Viongozi wa
kada mbalimbali, kuanzia ngazi ya Kijiji, Wilaya, Mkoa hadi Taifa, Kamati ina
maoni na mapendekezo yafuatayo:
MAONI:
-Kuhusu madai kwamba mauaji yanayotokea nchini yaundiwe tume,
Kamati imeona kuwa zipo sheria zinazotoa mamlaka ya kutafiti au kuchunguza
endapo kuna mashaka ya kifo hicho.
-Nafasi za Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa kiutendaji ziangaliwe
upya ili zisitumike na mhusika kwa ajili ya manufaa ya kisiasa.
-Kwa kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuwa ndiye mlinzi wa usalama
wa raia na mali zao, siasa za ubabe kwa vyama vya siasa ziepukwe kwa kuwa
zinaleta msuguano usio wa lazima na Jeshi la Polisi
-Kuhusu operesheni ya uzuiaji wa mkutano wa CHADEMA usio halali
Kijijini Nyololo tarehe 02 Septemba 2012, Jeshi la Polisi lilitekeleza wajibu
wake ipasavyo na kutumia nguvu sahihi. Operesheni iliyoandaliwa na kufanyika
ilikamilika kwa kuwatawanya watu waliofika kwenye mkutano, kukamata baadhi ya
Viongozi na wafuasi wa CHADEMA na hali ya utulivu ilirejea kwenye eneo husika.
MAPENDEKEZO
-Mauaji ya mwandishi wa habari Daud Mwangosi yalitokea baada ya
operesheni kumalizika, na amri ya kuondoka kwa askari eneo la tukio kutolewa na
Viongozi wa operesheni hiyo
-Jamii wakiwemo Viongozi waelimishwe umuhimu wa utii wa sheria,
kanuni na taratibu ili kudumisha amani na utulivu hapa nchini. Viongozi wengi
walionyesha hofu ya kuliingiza Taifa kwenye machafuko makubwa na uvunjifu wa
amani iwapo jamii haitazingatia umuhimu wa kutii sheria, kanuni, taratibu na
amri halali za Mamlaka.
-Msajili wa Vyama vya siasa afafanue majukumu ya vikundi vya
Ulinzi vya Vyama vya Siasa kama vile Green Guard, Red Brigade, Blue Guard.
-Iwepo programu mahususi ya Elimu ya Uraia nchini ili kujenga
uzalendo na kukuza maadili ndani ya jamii wakiwemo viongozi wa kada mbalimbali.
Hivi sasa jamii inashuhudia kutoweka kwa uzalendo na kuwepo kwa mmomonyoko wa
maadili ndani ya jamii.
Njia zifuatazo zitumike:
- Elimu ya uraia iimarishwe katika mitaala ya elimu kuanzia Shule
za msingi hadi Vyuo Vikuu.
- Uamuzi wa kurudisha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa vijana
utekelezwe mapema.
- Vyama vya Siasa, Madhehebu ya Dini, Tasnia ya Habari na Taasisi
zisizokuwa za Serikali zishiriki kikamilifu katika uenezi wa Elimu ya Uraia
nchini.
- Kuhimiza uzingatiaji wa weledi katika utendaji kazi kwa mujibu
wa taaluma na miongozo inayotolewa kuleta ufanisi. Aidha elimu endelevu sehemu
za kazi itiliwe mkazo.
-Kufanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya 1992
ili kuweka wazi shughuli za Vyama vya Siasa baada ya Uchaguzi Mkuu. Lengo ni
kuwa Shughuli za Siasa zihamie Bungeni kujadili na kuhoji mipango ya Serikali
na matumizi ya rasilimali za nchi. Kwa kufanya hivyo wananchi watapata nafasi
kufanya kazi za maendeleo.
-Kuboresha Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, hususan
uanzishwaji wa ofisi ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kuratibu ushirikiano/mahusiano
baina ya serikali (Jeshi la Polisi) na Vyama vya Siasa. Lengo ni kukuza
mahusiano na kuondoa mgongano.
-Utaratibu wa kufanya mikutano mara kwa mara kati ya Jeshi la
Polisi na Vyama vya Siasa, Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari uimarishwe
ili kujenga mahusiano mazuri na kupata ufumbuzi wa haraka kwa matatizo
yaliyojitokeza.
- Jeshi la Polisi nchini ni chombo muhimu katika ulinzi na usalama
wa raia na mali zao. Muundo uliopo wa Jeshi la Polisi uangaliwe upya Kisheria
ili kuziba mianya inayotoa nafasi kwa wanasiasa kulitumia Jeshi hilo kwa
manufaa ya Kisiasa. Aidha mipango ya kuboresha utendaji kazi kitaaluma iliyopo
hivi sasa upewe msukumo stahiki hususan rasilimali watu na fedha.
- Wananchi wahamasishwe kushirikiana na Polisi Jamii na Ulinzi shirikishi.
Polis ishirikiane na Serikali za mitaa kufanikisha malengo hayo.
- Jeshi la Polisi liimarishwe ili litekeleze majukumu yake
kikamilifu na kujenga mahusiano sahihi kati yake na Jamii, Vyama vya Siasa,
Tasnia ya Habari na Asasi zisizo za Kiserikali.
-Taasisi za habari zinazosimamia maadili na weledi wa vyombo vya
habari, hususan Baraza la Habari Tanzania na Jukwaa la Wahariri wafanye
utaratibu unaostahiki wa upatanishi kati ya waandishi wa habari, Jeshi la
Polisi na uongozi wa mkoa wa Iringa. Hii itasaidia kurejesha uhusiano mzuri
kati ya vyombo hivyo muhimu katika mkoa.
-Waandishi wa habari wapewe mafunzo ya jinsi ya kuripoti matukio
ya hatari/ghasia.
-Waandishi wa habari wavae vivazi maalum vya kuwatambulisha wakiwa
katika matukio hasa kwenye maeneo hatarishi.
-Waandishi wa habari wafanye kazi kwa weledi, uadilifu, uwazi na
wasijibainishe na vyama vya siasa.
-Kamati ya Ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa
Habari iliyoanzishwa mwaka 2008 ifufuliwe. Na kamati hizo ziteremke hadi kwenye
ngazi ya mkoa kama ilivyokuwa awali.
-Viongozi wa Polisi wanapotoa taarifa za tukio, ziwe zimefanyiwa
utafiti wa kina ili zisipotoshe jamii.
-Kuwe na jukwaa la mazungumzo ya mara kwa mara kati ya Jeshi la
Polisi na Vyama vya Siasa ili kila upande ujue wajibu wake na wa taasisi
nyingine katika kudumisha amani ya nchi na utamaduni wa kuheshimu sheria
zilizopo na kupunguza migongano.
9.0. CHANGAMOTO
Changamoto zilizojitokeza katika Uchunguzi zimegawanyika katika
mtiririko ufuatao:-
9.1 Jeshi la Polisi:
- Ukosefu wa Mafunzo endelevu.
- Ukosefu wa Uvumilivu katika utekelezaji wa Majukumu.
-Uelewa mdogo wa Elimu ya Uraia.
- Mmomonyoko wa Maadili.
- Kukosekana kwa uzalendo.
- Ukosefu wa Utii wa Sheria, Kanuni na Taratibu
9.2 Vyama vya Siasa:
- Kukosekana kwa uvumilivu katika kuendesha shughuli za Siasa.
-Kukosekana kwa Elimu ya Uraia
- Uelewa mdogo wa baadhi ya Viongozi wa Vyama kuhusu uendeshaji wa
Vyama vya Siasa.
- Ukosefu wa Sera/Mwongozo kwa Vyama vya Siasa kuendesha shughuli
za Kisiasa baada ya uchaguzi mkuu.
- Kukosekana kwa Jukwaa linalokutanisha mara kwa mara Vyama vya
Siasa na Jeshi la Polisi
- Mmomonyoko wa Maadili.
- Suala la Uzalendo.
- Ukosefu wa Utii wa Sheria, Kanuni na Taratibu
9.3 Jamii:
- Elimu ya Uraia.
- Mmomonyoko wa Maadili.
- Kukosekana kwa uzalendo.
- Ukosefu wa Utii wa Sheria, Kanuni na Taratibu.
26
10 HITIMISHO
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake
aliwahi kusema kuwa, “ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne ambavyo ni watu,
ardhi, siasa safi na uongozi bora. Watanzania kila mtu mahali pake, tunahitaji
kuwa na siasa safi yenye kujenga ustawi, tija, mshikamano, amani, maendeleo na
afya kwa taifa letu”.
Utulivu na amani kwa ajili ya mustakabali wa taifa, imekuwa ni
kauli mbiu ya viongozi mbalimbali ambao Kamati hii imepata fursa ya kuzungumzia
juu ya hali ya siasa na mahusiano yaliyopo baina ya Serikali, (Jeshi la Polisi,
Kamati za Ulinzi na Usalama wilaya na mkoa), vyama vya siasa, viongozi wa dini
na wananchi.
Wananchi na Viongozi wanataka kuona shughuli za siasa ya vyama
vingi inaendeshwa kwa hoja zenye tija badala ya vurugu na utengano. Njia
mojawapo ya kukabiliana na hali hii inayojitokeza ni kujenga uzalendo, maadili
mema, na mshikamano ili Tanzania iendelee kuwa kisiwa cha amani na utulivu.
Kamati hii inashauri na kupendekeza kuwa maoni haya yazingatiwe na
kutekelezwa.
Aidha Kamati imefaidika sana kupata fursa ya kukutana na viongozi
mbalimbali kuanzia kijiji hadi taifa na walitoa ushirikiano wa dhati katika
kutoa mchango wao wa mawazo. Kamati inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt Emmanuel Nchimbi (Mb) kwa imani yake kwa
wajumbe wa Kamati ya Uchuguzi.