Monday, August 6, 2012


  HABARI ZA LEO
 
6/08/2012
 

ASKARI ALIYEWALIPUA WENZAKE MOROGORO ADAIWAKUJINYONGA

Wananchi wakishuhudia mwili wa ‘Dunga’ .
Mwili wa Donald Mathew ‘Dunga’ ukiondolewa mtini.
Mwili wa Donald Julius ukibebwa kupelekwa kwenye gari la polisi.
...Ukiingizwa kwenye gari la polisi.
Barua ya Dunga kwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
ASKARI jasiri aliyejizolea sifa mkoani hapa kwa kitendo chake cha kuwataja hadharani baadhi ya askari wenzake akiwashutumu kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kushirikiana na majambazi kufanya uharifu, Donald Julius Mathew, mwenye namba ya jeshi la polisi F3276 amekufa akidaiwa kujinyonga.
Mwili ya afande huyo ambaye ni maarufu mkoani hapa kwa jina la Dunga umekutwa ukiningin'ia juu ya mti eneo la Daraja la Shani ambalo liko katikati ya Mji wa Morogoro.
Dunga aliwalipua maafande zaidi ya sita ambao walihamishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema na yeye kuhamishwa mkoa wa Singida.
Hata hivyo, Dunga aligomea uhamisho huo akipinga watuhumiwa kutochukuliwa hatua.
Sababu alizotoa Dunga zinaelezwa katika barua aliyomwandikia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyoitoa kwa mtandao huu na ambayo tunaichapisha.

KOZI YA UTAWALA IMEFUNGULIWA RASMI NA RAIS WA TFF

 

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amefungua rasmi Kozi ya Uongozi na Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoanza leo Agosti 6 mwaka huu Msimbazi Center jijini Dar es Salaam.
Kozi hiyo ina washiriki zaidi ya 30 itamalizika Agosti 11 mwaka huu na itaendeshwa na Wakufunzi kutoka FIFA na imefunguliwa leo saa tatu asubuhi.

Wakufunzi hao ni Barry Rukoro anayetoka Namibia, Henry Tandau (Tanzania) na Senka Kanyenvu (Botswana).

YANGA WATUA BUNGENI KWA MBWEMBWE, SPIKA, WAZIRI MEMBE WAWAPONGEZA LAKINI RAGE AWAPIGA DONGO...!!

Anaelewa 'kuhusu utaratibu'? 'Mwongozo wa Spika'? Kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintief (mbele kulia) akifuatilia shughuli za bunge leo wakati yeye na wachezaji wake (nyuma) walipotinga 'mjengoni' kulionyesha kwa wabunge mjini Dodoma Kombe la Kagame walilotwaa kwa mara ya pili mfululizo. Yanga wamekwenda bungeni baada ya kualikwa na wabunge walio wanachama wa Yanga.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia taji lao la ubingwa wa Kombe la Kagame hivi karibuni... kombe hilo limetambulishwa kwa wabunge mjini Dodoma leo
Woten hawa wametinga na kombe la Kagajme kwenye mjengo wa Bunge leo... kutoka kushoto ni Rashid Gumbo, Haruna Niyonzima, Said Bahanunzi (nyuma) na Hamis Kiiza wakishangilia baada ya kupata bao katika mechi yao ya fainali ya Kagame dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi karibuni
Kikosi cha klabu ya Yanga kimetua kwa kishindo ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo na kuibua shangwe na nderemo kutoka kwa wabunge mashabiki wa timu hiyo wakati wakitambulisha kombe walilotwaa hivi karibuni la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu Kombe la Kagame.
Baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, wachezaji wa Yanga walioongozana na mwenyekiti Yusuf Manji, Makamu MwenyekitiClement Sanga, mjumbe wa bodi ya wadhamini, Mama Fatma Karume na Francis Kifukwe walitambulishwa na bungeni na kupongezwa na Spika wa Bunge, Mhe. Anna Makinda.
Kufuatia tukio hilo, wabunge waliripuka kwa shangwe na bashasha tele, huku wale ambao wanafahamika kuwa ni mashabiki wa Simba, kama Mhe. Ismail Aden Rage ambaye pia ni mwenyekiti wa wekundu hao wa Msimbazi, wakionekana kushangilia vilevile, lakini kwa namna ya utani zaidi.
Baada ya utambulisho wa msafara wa wachezaji wa Yanga, wakiwamo nyota kama Haruna Niyonzima ‘Fabregas’, Hamis Kiiza na mfungaji bora wa michuano ya Kagame, Said Bahanunzi, likaja tukio la kuonyeshwa kwa kombe walilotwaa, la Kagame.
Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisimama na kombe hilo, akaenda mbele na kulipunga hewani huku akilielekeza kila upande ili wabunge wote wapate nafasi ya kuliona. Ushangiliaji wa kupiga meza ulitwaa nafasi na kuufanya ukumbi mzima urindime.
Hata hivyo, katikati ya kushangilia huko, wabunge wengi ambao ni mashabiki wa Simba, wakiongozwa na Rage, wakajibu mapigo ya wapinzani wao wa jadi kwa namna ya kuchekesha zaidi baada ya kunyoosha juu vidole vitano vya mkono; pengine wakikumbushia matokeo ya kichapo kikali cha mabao 5-0 walichowapiga Yanga katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara!
Baadaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe akawapongeza Yanga wakati akisoma hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha.
Membe ambaye pia ni mnazi wa Yanga, akasema kwamba atakuwa hajatenda haki kama hatawapongeza Yanga ambao wamekuwa mabalozi wazuri wa Tanzania kwa kutwaa ubingwa wa Kagame unaohusisha klabu bingwa za Afrika Mashariki na Kati; na kwamba amefurahi kuwa ujio wao bungeni umekuja katika siku mwafaka ambayo wizara yake inawasilisha bajeti ya mwaka ujao wa fedha.
Yanga walitwaa kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo baada ya kushinda 2-0 katika mechi yao ya fainali dhidi ya Azam FC.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUTURISHA IKULU NDOGO MJINI DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tano kutoka kulia) akijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika swala ya Magharibi wakati wa hafla ya Futari aliyowaandalia na kushiriki nao pamoja katika futari hiyo iliyoandaliwa Ikulu ndogo mjini Dodoma jana.

Makamu wa Rais, Dkt Bilal, akiagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Maliasili na Utalii, Hamis Kagasheki, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya waalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari, iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari, iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari, iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mhe. Juma Kapuya, ambaye alikuwa ni mmoja kati ya waalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari, iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana wageni wake na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya hafla ya futari, iliyoandaliwa na Makamu Ikulu Ndogo mjini Dodoma jana

TRAFIKI KUPANGWA MLIMA KITONGA ILI KUPUNGUZA AJALI ASEMA KAMANDA MPINGA

kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga (hayupo pichani)na askari wa kikosi hicho mkoa wa Iringa wakilitazama basi la kampuni ya Seth Star lenye namba za usajali T500 BEV likishuka kwa mwendo mkali mteremko wa Kitonga huku malim ya mataili yakitoa moshi kutokana na msuguano wa breck jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa abiria

KUTOKANA na ajali za mara kwa mara zinazoendelea kutokea katika mlima wa kitonga katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga amekiagiza kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa kuwekwa askari wa kutosha wa usalama barabarani (Trafiki) katika mlima huo.

Akizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com jana baada ya kutembelea eneo hilo la Kitonga na kushuhudia jinsi ambavyo mabasi ya abiria na malori ya mizigo yanavyopita kwa kasi bila tahadhari yoyote katika kona za mlima huo ambazo kimsingi ni kona kali ambazo madereva wanapaswa kuendeshwa kwa uangalifu wa hali ya juu.

Alisema kuwa kati ya maeneo yanayoongoza kwa ajali za mara kwa mara na kusababisha vifo vya watanzania ni pamoja na eneo hilo la mlima Kitonga hivyo bila kuwepo kwa mikakati ya haraka kutoka kikosi hicho cha usalama barabarani uwezekano wa kupunguza ajali hiyo bado utakuwa ni mdogo zaidi.

kamanda Mpinga alisema kuwa moja ya mikakati ambayo kikosi chake kilikuwa kikiitazama kuifanya kama njia ya kuepusha ajali eneo hilo ni pamoja na kukutana na wakala wa barabara mkoa wa Iringa (Tanroads) ili kuweka matuta katika eneo hilo ila mkakati huo baada ya kuufanyia utafiti wa kutosha wameona si njia nzuri ya kupunguza ajali kutokana na eneo hilo kuwa na mlima mkali hivyo wanahofu ukawa ni sehemu ya ajali hasa kwa magari yanayopandisha mlima huo.

Hivyo alisema mkakati rahisi ambao wanaona utasaidia kupunguza ajali za barabarani ni kukomesha matukio ya uharifu kwa madereva kuvamiwa na majambazi katika eneo hilo ni kuweka doria ya askari Trafiki ambao watatembea kwa miguu na wengine kufanya doria ya magari mara kwa mara katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na malori na magari yote ya abiria kukaguliwa kabla ya kuanza kushuka ama kupandisha eneo hilo la mlima na mteremkoa mkali wa Kitonga.

"Njia hii ya kukagua mabasi ya abiria na malori itasaidia kujua matatizo ya gari husika na iwapo litabainika kuwa ni bovu basi halitaruhusiwa kushuka wala kupanda eneo hilo la Kitonga hadi litakapo tegenezwa"

Kwani alisema kuwa ajali nyingi zinazotokea eneo hilo zinasababishwa na ubovu wa vyombo hivyo vya usafiri ama uzembe wa madereva kwa kutaka kuyapita magari mengine bila kutazama kona kali zilizopo katika eneo hilo.

Aidha alisema hata Tanroads mkoa wa Iringa inapaswa kuweza kuweka alama za kutosha za usalama barabara katika mlima huo ili kuwafanya madereva kuchukua tahadhari badala ya kuacha alama chache zilizopo kwa sasa.

MKUTANO WA CHADEMA LONDON‏

M4C LONDON
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA KINAPENDA KUWATANGAZIA WATANZANIA WOTE WAISHIO LONDON NA SEHEMU ZA JIRANI KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO WA UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA LONDON. TAWI AMBALO LITAFUNGULIWA NA MHESHIMIWA GODBLESS LEMA.
UFUNGUZI HUO UTAFANYIKA THATCHED HOUSE PUB ILIYOPO BARKING SIKU YA JUMANNE 07/08/2012 SAA MBILI USIKU.
KATIKA MKUTANO HUO PIA WATACHAGULIWA VIONGOZI MBALIMBALI WA CHADEMA TAWI LA LONDON .
TUNAWAOMBA WANACHADEMA WOTE WAJITOKEZE KWA WINGI KUJA KUHUDHURIA TUKIO HILI LA KIHISTORIA.
Venue ; Thatched House Pub
RIPPLE ROAD, BARKING, ESSEX, IG11 9PG Kwa maelezo zaidi wasiliana na chacha thomas 0712689297

AJALI MBAYA YA MALORI YAUA WANNE KITONGA IRINGA

Gari ya kampuni ya Asas Iringa ikijaribu kutoa msaada wa kuvuta malori yaliyogongana ili kutoa maiti iliyonabanwa na malori hayo
Hivi ndivyo malori hayo yalivyogangana eneo hilo la Kitonga leo
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga akiwa eneo la tukio
Askari polisi na wananchi wakitazama moja kati ya maiti zilizo naswa katika mabaki ya malori hayo
Mwili wa dereva wa lori ukiwa umebanwa katika eneo hilo la tukio
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga (kushoto) akiwa eneo la ajali mlima Kitonga leo

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga akipandisha mlima kutoka katika korongo la mlima Kitonga Iringa akitoka kushuhudia ajali mbaya ya malori mawili yaliyogongana na kutumbukia korongoni na kupelekea vifo vya watu wanne papo hapo usiku wa kuamkia leo

Wananchi mbali mbali pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa (hayupo Pichani) MOhamed Mpinga wakitazama malori mawili yaliyogongana katika mteremko wa Kitonga Iringa usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya watu wanne baada ya kutumbukia katika korongo
HUKU mkoa wa Iringa ukiwa umepewa hadhi ya kuwa mwenyeji wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani kwa mwaka huu ,mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda ashuhudia ajali mbaya iliyopelekea vifo vya watu wanne kufa papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana na kutumbukia bondeni katika mteremko wa mlima kitonga wilayani Kilolo katika barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam .

Hata hivyo dereva wa lori bovu ambalo lilikuwa limeegeshwa eneo hilo alipona katika ajali hiyo .

Akizungumza katika eneo la ajali mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga alisema kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia jana na kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T587 BGP aina la scania ambalo lilikuwa na mali mbali mbali za dukani lilikuwa limeharibika na kuegeshwa kando ya barabara hiyo kugongwa na lori lenye namba za usajili T T319 BDG aina ya Scania ambalo lilikuwa limebeba shaba kuligonga lori lililokuwa limeegesha kando ya barabara hiyo.

Mpinga alisema kuwa katika ajali hiyo watu wanne walikufa papo hapo na mmoja ambaye ni kijana alijeruhiwa vibaya na kuwa miongoni mwa waliokufa ni pamoja na mwanamke mmoja ambaye inasadikika ni mkazi wa wilaya ya kilolo aliyekuwa amepanda katika lori hilo .

Alisema kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha ni pamoja na utingo wa lori ambalo lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara hiyo ambalo lilikuwa limebeba mali za dukani ambaye alikuwa nje ya lori hilo akifanya mawasiliano ya simu na mwenzake na hivyo kugongwa na lori hilo la Shaba ambalo breck zilionyesha kuwa na matatizo.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na ajali hiyo kutokea Agosti 4 majira ya jioni ila zoezi la utoaji wa maiti ya dereva wa lori hilo lenye shaba bado ni gumu kutokana na mwili wa dereva huyo kubanwa vibaya ya tela la lori hilo lenye shaba .

Alisema kuwa kabla ya tela hilo lenye shaba kufunika kibini ya lori hilo kebini hiyo ilikatika na kutangulia korongoni na baada ya hapo tela lenye shaba kufuata nyuma na kutua juu ya kibini hiyo.

kamanda huyo alisema kuwa ajali hiyo imetokea wakati mkoa wa Iringa unataraji kuwa mwenyeji wa wiki ya nenda kwa usalama ambayo kitaifa itafanyika katika mkoa wa Iringa huku akiwataka madereva kuheshimu sheria za usalama barabarani kama njia ya kuepuka ajali kama hizo.

Aidha alisema kuwa kutokana na eneo hilo la mlima wa Kitonga kuendelea kuwa na eneo maarufu kwa ajili tayari mkakati umewekwa kwa ajili ya kuongeza ulinzi en eo hilo pamoja na kufanya doria za mara kwa mara za miguu ya magari kwa askari wa usalama barabarani ili kusaidia kupunguza ajali katika eneo hilo.

Alisema kuanzia sasa askari wa usalama barabara watawekwa eneo hilo ili kuweza kukagua magari yote ya abiria na mizigo ili kabla ya kushuka mteremko huo kuwa na uhakika wa breck kama njia ya kuanza kuchukua hatua za kukabiliana na ajali mbaya katika mteremko huo.

MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA ILALA JERRY SILAA ARUDISHA FOMU ZA UVCCM - NEC.

Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa akirejesha fomu za kugombea nafasi ya ujumbe wa UVCCM-NEC katibu wa UVCCM mkoani Mwanza. Bw. Elias Mpanda, katika ofisi za CCM mkoani- Jijini Mwanza. Mstahiki meya Manispaa ya Ilala Bw. Jerry Silaa anagombea nafasi ya ujumbe wa UVCCM-NEC ngazi ya taifa.
Mstahiki meya aliweka wazi nia yake ya kutaka kuwawakilisha vema vijana wa kitanzania kwenye UVCCM-NEC na aliwaasa vijana wengine kushiriki kwenye mchakato huo na huku akisisitza kwamba yuko tayari kufanya kazi kokote nchini kwa maslahi ya wananchi, vilevile meya aliwaasa viongozi wote kuwajibika na kutimiza ahadi zao walizozitoa kwa wananchi na kwa kuweka mbele maslahi ya taifa na sio yao binafsi

SBL Moshi wamuaga aliyekuwa mkurugenzi wao Richard Wells

Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (katikati) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (kulia) na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Richard Wells wakati wa tafrija maalum ya kumuaga Wells iliyofanyika Kiwanda cha SBL mjini Moshi hivi karibuni.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wapili kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (wapili kulia) na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Richard Wells (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL Teddy Mapunda wakati wa tafrija maalum ya kumuaga Wells iliyofanyika Kiwanda cha SBL mjini Moshi hivi karibuni.
Mama Tundu Pinda akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL aliyemaliza muda wake, Richard Wells wakati wa tafrija ya kumuaga iliyofanyika kiwanda cha SBL mjini Moshio hivi karibuni.
Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi mpya wa SBL, Steven Gannon
Richard Wells (kushoto) akiwa akitika vazi la jadi la jamii ya Wamasaa pamoja na Kisu jamii ya sime alilokabidhiwa na Wafanyakazi wa SBL mjini Moshi wakati walipomuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake na kumkaribisha Mkurugenzi Mpya Steven Gannon.
Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Bia Serengeti Mjini Moshi wakipiga picha na viongozi wao.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wapili kushoto) akiwa katika Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Steve Gannon (kulia) na Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Richard Wells (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Dr. Msengi
Mkurugemzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda akitunzwa na Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji wa SBL, Nandi Mwiyombela kwa kutoa burudani ya aina yake wakati wa tafrija hiyo ya kumuga Richard Wells.
Vijana wa Kalunde Band wakiwa kazini kutoa burudani
Hapa kazi tu.....Mkurugemzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapundana Mkurugenzi wa Masoko Epraim Mafuru wakiimba wakati wa tafrija hiyo ya kumuaga Richard Wells.
Richard Wells akicheza mziki na Wafanyakazi wa Kiwanda cha SBL mjini Moshi wakati wa tafrija ya kumuaga.
Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa SBL, Steven Gannon akisakata rumba na wafanyakazi wa SBL Kiwanda cha Moshi.
Wafanyakazi wakiwa wanaendelea na vitu vya hapa na pale wakati wa tafrija hiyo ya mkumuga Mkurugenzi Mtendaji aliyemaliza muda wake Richard Wells mjini Moshi.

FOMU ZA KUGOMBEA NAFASI YA UWT TAIFA ZAANZA KURUDISHWA

Mgombea nafasi ya Mwenyekiti UWT Taifa Bi, Halima Mohamed Mamuya kulia akirudisha fomu ya kuomba kugombea nafasi hiyo kwa Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni UWT Makao Makuu Bi Riziki Kingwande Dar es salaam leo
 

No comments:

Post a Comment