MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba amesema
jumuiya hiyo ya wanawake wa CCM, imejipanga kuhakikisha mgombea urais wa
chama hicho, Dk John Magufuli anashinda katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba
25 mwaka huu.
“UWT tumejipanga kama mnavyojua sisi ni jeshi kubwa na tutahakikisha tunampeleka Magufuli Ikulu... Leo (jana) tuna kikao kizito sana cha kuweka mikakati ya kumpeleka Magufuli Ikulu,” alisema Simba jana mkoani hapa. Tayari UWT imeshatoa kaulimbiu katika uchaguzi huo, inayosema ‘Wanawake jeshi kubwa, Magufuli Ikulu ni lazima’.