Thursday, June 7, 2012


TANGAZO LA MKUTANO WA HADHARA WA CHAMA CHA MAPINDUZI UTAKAOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI, SIKU YA JUMAMOSI, TAREHE 09-06-2012.


TANGAZO:
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kimeandaa Mkutano Mkubwa wa Hadhara kwa wananchi wote, Siku ya Jumamosi, tarehe 09/06/2012, Katika Viwanja vya Jangwani Kuanzia saa 8 mchana.
Maudhui; “ Kutoa Msimamo Wake Juu ya Masuala Yanayogusa Mustakabali wa Taifa. Hivyo Chama Kitatumia Fursa hiyo Kuelezea Watanzania Juu ya Msimamo Wake Katika Mambo yafuatayo:
1. Hatma ya maisha ya Watanzania
· Ajira
· Miundo mbinu ya Barabara, Reli, Bandari Na Anga.
· Bei za bidhaa mbalimbali.
· Umeme
· Rasilimali za taifa
2. Msimamo wa Chama Cha Mapinduzi kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya.
3. Vurugu za Zanzibar.
Katika Mkutano huo, Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali watakuwepo na kutoa ufafanuzi juu ya masuala hayo yaliyoainishwa kama msimamo wa Chama Cha Mapinduzi.
Chama Cha Mapinduzi, kinawaalika wanachama wake wote, wakereketwa na wananchi kwa ujumla kuhudhuria katika mkutano huo mkubwa. Mkutano utafanyika kwa amani na utulivu na wote mnakaribishwa.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na:
JUMA SIMBA
KATIBU WA SIASA NA UENEZI
MKOA WA DAR ES SALAAM.
07/06/2012

JAMAA WAKUTANA NA ADHA YA WANAJESHI ALMAARUFU KAMA WAJEDA.

Kila siku mnaambiwa msipite maeneo yao hawa jamaa lakini raia hamkomi.
wanajeshi walivyo msuba.............inaweza ndio ikawa shughuli ya siku nzima.........mkacheza kiduku hapooo hadi maji yatakapokauka............hawana tatizo na mtu, watapeana zamu ya kwenda kula ila raia ndio mtakausha huo Mto. 

KCB TANZANIA YAZINDUA HUDUMA MPYA YA DISPORA BANKING

Mwenyekiti Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania DK Edmund Mndolwa akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya KCB DIASPORA BANKING uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akizindua rasmi huduma mpya inayotolewa na KCB DIASPORA BANKING, Katikati ni Mmoja wa Mameneja wa benki hiyo SHOSE KOMBE. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo MOEZ MIR.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa huduma mpya ya KCB DIASPORA BANKING iliyoanzishwa na benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya KCB Tanzania Christine Manyenye akifafanua kuhusiana na huduma mpya iliyoanzishwa na benki hiyo ya KCB DIASPORA BANKING wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa huduma mpya ya KCB DIASPORA BANKING iliyoanzishwa na benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Sakata la Mafuta Jijini Mbeya: Mafuta ya Taa Jijini Mbeya ya panda bei kutoka Tsh 2175 mpaka kufikia Tsh 3000 na 3500. Ni Kutokana na uhaba wa Mafuta hayo.

Wananchi wa Jiji la Mbeya wakiwa wana haha kupata Mafuta ya taa katika kituo cha mafuta
Baadhi ya Njinga zikiwa zimepaki eneo ambalo ndilo pekee Mafuta yanapatikana jinini Mbeya
Mdau akiwa anatazama vema kama anazo pesa za kununua Mafuta hayo baada ya kushtuka kuambiwa kuwa bei imepanda mpaka kufikia 3500
Kila mtu anataka kupata mafuta kwa muda katika eneo hilo Mpaka wenye mapipa nao wamo.

KITUKO KUTOKA KWENYE AKAUNTI YA FACE BOOK YA JOHN KITIME LEO!

Mwanamuziki nguli John Kitime
Joji alikuwa shule ya vidudu na akaanza kujua hesabu. Mjomba wake akaja;
JOJI: Mjomba najua hesabu.
MJOMBA: Tatu kujumlisha mbili?..Mtoto akaanza kuhesabu vidole akamaliza;
JOJI: Tano
MJOMBA: Haya sasa sitaki uhesabu vidole. Tia mikono yako kwenye mifuko ya kaptura. Haya tano kujumlisha tano?....mtoto akaanza kuhesabu vidole mfukoni.
JOJI: Kumi na moja!!
Haaaa haaaa haaaa haaaaa!!!! Joji you are Very Bright!

KAMATI ZA BUNGE ZAENDELEA NA KAZI YA KUPOKEA MAKADIRIO YA BAJETI ZA WIZARA LEO


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufunzo Mhe. Shukuru Kawambwa akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara yake mbele ya Kamati ya Huduma za Jamii kabla ya kupelekwa Bungeni. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii Mhe. Magareth Sitta na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Faustine Ndugulile.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Jamii Mhe. Faustine Ndugulile (kushoto) na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Magareth Sitta (katikati) wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufunzo Mhe. Shukuru Kawambwa alipokuwa akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara yake mbele ya kamati hiyo leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Jenister Mhagama akisisitiza jambo wakati wakipokea makadirio ya bajeti ya wizara ya kazi na Ajira iliyo wasilishwa mbele ya kamati hiyo. Kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Juma Nkamia na Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Chacha Nyakega, Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka na naibu waziri wa Wizara ya kazi na Ajira Mhe. Dkt Milton Makongoro Mahanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya fedha na Uchumi Mhe. Andrew Chenge akifafanua jambo mbele ya wajumbe wakamati na watendaji kutoka wizara ya fedha baada ya kupokea mapendekezo ya bajeti ya wizara ya fedha yaliyo wasilishwa mbele ya kamati hiyo leo. Kulia kwake ni Waziri wa fedha Mhe. William Mgimwa Mhe Saada Mkuya Salum na Mhe Janet Mbene, amabo ni Manaibu waziri katika wizara hiyo.
Mjumbe wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma Mhe.Murtaza Ally Mangungu akifurahia jambo baada ya kupokea hesabu zilizokaguliwa za chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa mwaka 2010/2011. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. zitto Kabwe na Kushoto ni Katibu wa Kamati hiyo Erick Maseke
kamati ya POAC ikiendelea na kazi.
Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

AUWA NA KISHA KUNYOFOLEWA UUME, NA MIKONO MKOANI ARUSHA


KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA ARUSHA LIBERATUS SABAS
(NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA)
Mtu mmoja ambaye hajajulikanan jina lake amefarikidunia huku baadhi ya viungo vyake hasa sehemu za uume wake zikiwa zimechomolewa pamoja na mikono yake
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa arusha Sabas Liberatus alisema kuwa tukio hilo lilitokea may 26 majira ya saa tni asubuhi katika eneo la Mto Nambala wilyani Arumeru
Kamanda Sabas alisema kuwa katika siku ya tukio mytu mmoja mwenye jinsia ya kiume ambaye hajatambulika mpaka sasa anakadiriwa kuwa na miaka25-30 alikutwa akiwa amefariki
Kamanda huyo aliongeza kuwa mara baada ya wapita njia kumkuta akiwa amefariki waligundua kuwa pia hana viungo mbalimbali ndani ya mwili wake hali ambayo ilizua tafrani kubwa
‘hawa watu walipomuangalia kwa undani sana waliweza kujua na kutambua kuwa baadhi ya viungo vyake havipo na ndipo walipota taarifa kwa jeshi la polisi na sisi tulipoofika ndani ya eneo la tukio tuliyakuta hayo hayo”alisema Kamanda Sabas
Pia aliongeza kuwa baada ya polisi kufika katika eneo la tukio walikuwa mwili huo ukiwa na suruali aina ya jeans ambayo ilikuwa imeshushwa hadi chini ya magoti na viungo vyake vikiwa vimenyofolewa
Hataivyo jeshi hilolinaendela na upelelezi juu ya tukio hilona upelelzi wa kumfahamu chanzo cha umati huo huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mount Meru

Waziri akizungumza na Kamati ya Bunge

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akizungumza na Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira kwenye ukumbi wa Hazina kulia Mwenyekiti wa Kamati hiuo James Lembeli kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga,Naibu katibu Mkuu Eng Ngosi Mwihava,Mh Zakhia Megji kikao hicho kimefanyika leo Mjini Dar es Salaam[Picha na Ali Meja

Baraza la Sanaa (BASATA) lawapa somo waandaaji wa Epic Bongo Star Search 2012





Na Mwandishi Wetu

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeendesha semina ya siku moja kwa majaji wa shindano la Epic Bongo Star Search 2012 kwa kuwataka kuzingatia maadili ya kazi zao.

Akitoa somo kwa majaji hao mratibu wa matukio wa Basata Malimi Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa asilimia kubwa ya washiriki wanategemea zaidi msaada wao katika kukuza vipaji.

Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa mazingira waliyotoka washiriki na kuangalia namna ya kuwasaidia kulingana na mikoa yao kwa kuwa wapo ambao wana vipaji lakini wanatatizwa na suala la kuyazoea mazingira.

Alisema kuwa kwa kuwa mwaka huu EBSS itaruhusu washiriki wa miaka 16 hivyo ni vema zaidi wakazingatia suala la sauti kulingana na umri wa mshiriki sababu watakuwepo wenye sauti za kitoto pia.


Pia aliwataka majaji hao kuhakikisha kuwa hawatoi aina yoyote ya upendeleo na wala kuwa karibu zaidi na baadhi ya washiriki wa shindano hilo.

Pia alisisitiza kuwa majaji wanalo jukumu kubwa la kuwaelekeza namna ya kuimba, kuvaa, kujiheshimu na usafi wa mwili pia.

“Hiii ni semina ya kuwekana sawa tu kwa kuwa hili shindano lipo kwa muda mrefu na majaji mmekuwa mkifanya vema, kwa niaba ya BASATA napenda kuchukua muda huu kuwataka muwe makini katika kuzingatia maadili haya niliyoyasema na hata mengine pia”alisema Mashili.Naye Mkurugenzi wa Berchmark Production inayoandaa shindano hilo Ritha Paulsen alisema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa majaji kwa kuwa muda mzuri wa kukumbushana mambo muhimu yahusuyo muziki.

Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 16 katika ukumbi wa Royal Village.

Majaji wa shindano hilo waliohudhuria ni pamoja na Jaji Mkuu Ritha Paulsen, Master Jay, Salama pamoja na mratibu wa EBSS kutoka Basata Vicky Temu.


MWENYEKITI WA KLABU YA SIMBA ASEMA: MKATABA WA YONDAN YANGA NI BATILI


Simba Sports club imesikitishwa na kitendo cha Young Africans kuvunja taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patric Yondani kwa kuzungumza naye na baadae kwa ushahidi wa picha kuonekana wakimuandikisha makaratasi ambayo baadae imeripotiwa na vyombo vya Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Young Africans.
Kwamba katika picha hiyo ameonekana mjumbe wa Young aliyejiuzuru bwana Seif Ahmed na hilo lilitoa shaka kama utaratibu huo umefanywa na klabu ya Young, lakini shaka hiyo imeondolewa pale ambapo tovuti ya Young imetangaza kumsajili mchezaji huyo wa Simba SC, lakini zaidi ya hilo picha inaonyesha fedha zikiwa zimewekwa mbele ya mchezaji jambo linaloonyesha mazingira ya kurubuniwa kwani kwa utaratibu wa kifedha, pesa nyingi kiasi hicho malipo yake yanashauriwa/yanapashwa kupitia benki.
Mbali ya hayo picha hiyo inamuonyesha Kelvin akiwa katika jezi ya mazoezi ya timu ya Taifa na yenye logo ya Kilimanjaro na kumbukumbu zinaonyesha mkataba kati ya TBL na TFF tarehe 9/5/2012, kwa haraka haraka tukio hilo limefanyika katika kipindi chini ya mwezi mmoja ingawa taarifa za ushahidi zinaonyesha tukio hilo limetokea jana tarehe 6/6/2012.
Simba Sports Club ilipenda kuamini kwamba tukio hilo haliihusu klabu ya Young kwani bwana Seif Ahmed alishajiuzuru kutoka kwenye kamati ya Young Africans, kwani Young ni klabu kongwe na inayojua taratibu zote za usajili.
Kwamba Simba Sports Club imeshawasiliana na jopo lake la mawakili na inajiandaa kuishtaki klabu ya Young katika chombo husika cha mpira na kudai adhabu ya kutopitisha majina yote ya usajili ya Young kwa mwaka 2012/2013 na miaka mingine miwili ijayo na Simba SC ipo tiyari kufuatilia suala hili hadi katika mahakama ya mpira ya FIFA.
Kelvin Yondani ni mchezaji halali wa Simba Sc aliye na mkataba hadi 31 mei 2014 mkataba ulioongezwa tarehe 23/12/2011 kuundeleza mkataba wa awali uliokuwa unaisha tarehe 31/5/2012. Sheria za FIFA za hadhi na uhamisho wa wachezaji ziko wazi katika kipengele cha 5 kifungu kidogo cha 2 kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja tu kwa wakati mmoja.

Imetolewa   tarehe 7/6/2012.
MH. ISMAIL ADEN RAGE (MB)
MWENYEKITI
SIMBA SPORTS CLUB

Rais Dk. Shein akutana na Balozi wa Msumbiji na Sweden


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali
Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania Amour
Zakaria aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,kwa kumaliza muda
wake wa kazi nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali
Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania Amour
Zakaria aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,kwa kumaliza muda
wake wa kazi nchini.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Sweden Nchini
Tanzania Lennarth Hjelmaker,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar
kujitambulisha kwa Rais.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini
Tanzania Lennarth Hjelmaker,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar
kujitambulisha kwa Rais.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

RAIS KIKWETE AAGANA NA BALOZI WA CANADA


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo Juni 7, 2012 katika Ikulu ya Dar es salaam
amekutana na kuagana na Bw Robert J. Orr, Balozi wa Canada nchini, anayemaliza muda wake wa uwakilishi.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Bw Robert J. Orr, Balozi wa Canada nchini, anayemaliza muda wake wa uwakilishi.

GAMBIA KUWASILI LEO USIKU TAYARI KWA MPAMBANO WAO NA TAIFA STARS



Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) ambayo awali ilikuwa iwasili nchini leo (Juni 7 mwaka huu) saa 1.40 asubuhi sasa itawasili leo saa 9.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.
The Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku lakini kukawa na ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya ambapo ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es Salaam.
Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 22 wakiwemo tisa wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi hiyo kitafikia kwenye hoteli Sapphire iliyopo Mtaa wa Lindi na Sikukuu eneo la Kariakoo.
Wachezaji walioko katika msafara huo ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay na Demba Savage.
Wengine ni Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.
PROGRAMU YA MAZOEZI YA GAMBIA
IJUMAA JUNI 8
01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa
JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
10.00 jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti Wa CUF Profesa ibrahim Lipumba Wahudhuria Mazishi Ya Mwenyekiti Mstaafu Wa CUF Marehemu Musobi Mageni

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akitoa salaam za pole kwa viongozi na chama cha Wananchi CUF na wananchi wa mkoa wa Mwanza katika mazishi ya Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, marehemu Musobi Mageni
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiweka udongo kwenye kaburi la Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, marehemu Musobi Mageni ,kulia kwake ni Mwenyekiti wa Cuf Profesa ibrahim Lipumba ambao wote walijumuika na viongozi na chama cha Wananchi CUF na wananchi wa mkoa wa Mwanza katika mazishi ya Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, marehemu Musobi Mageni
--
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amejumuika na viongozi wa chama cha Wananchi CUF na wananchi wa mkoa wa Mwanza katika mazishi ya Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, marehemu Musobi Mageni huko kijijini kwao Ngudu, Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Katika mazishi hayo, pia alihudhuria Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, Makamu Mwenyekiti, Machano Khamis Ali, pamoja na wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa, wakiwemo Waziri wa Afya Zanzibar, Juma Duni Haji na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Haki za Binaadamu, Salum Bimani.
Marehemu Musobi alifariki Dunia Mei 30, mwaka huu nyumbani kwake Ngudu baada ya kusumbuliwa na maradhi ya shinikizo na damu na sukari kwa muda mrefu.
Marehemu alihamia chama cha Wananchi CUF mwaka 1994 na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Taifa mwaka 1995 hadi 1999 alipostaafu na kubaki kuwa Mjumbe wa kudumu wa Baraza Kuu la Taifa na Mkutano Mkuu wa chama hicho hadi kifo chake.
Katika uhai wake, marehemu aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini kuanzia mwaka 1972 hadi 1975, mwaka 1976 hadi 1978 Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Rajan Industries Ltd. Nafasi nyengine ni alizowahi kushikilia ni Ubunge na Mkuu wa Wilaya katika wilaya ya Chunya, Kahama na Muleba.
Akitoa salamu za rambirambi, Makamu wa Kwanza wa Rais, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakati wa mazishi alisema, marehemu alikuwa kisima cha busara na mwenye hekima kubwa na ndio maana viongozi wa CUF walikuwa wakikimbilia kwake kuchota ushauri wake.
“Huu ni msiba mkubwa sio tu kwa familia yake, bali kwa chama chetu na kwa serikali zote mbili”, alisema Maalim Seif.
Marehemu ambaye alizaliwa mwaka 1930, ameacha wajane wawili, watoto 15, wajukuu 28 na vitukuu sita.
Na
Khamis Haji
Ofisi Ya Makamu wa Kwanza Wa Rais Zanzibar

MILIONI 421.8 ZAPATIKANA KUCHANGIA MPANGO WA ELIMU KATA YA KIPAWA JIJINI DAR ES SALAAM

Mbunge wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (kulia), Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) na Mwenyeji wa harambee ya kuchangia mpango wa elimu wa Kata ya Kipawa, Diwani wa Kata hiyo Bonah Kaluwa, wakimuongoza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi kuingia ukumbini Katika hafla iliyofanyika jana usiku ndani ya hoteli ya Kilimanjaro (Kempiski hotel) jijini Dar es Salaam .
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo
Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akitoa neno la shukurani kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Mgeni rasmi wa Hharambee hiyo akimpa mkono wa asante mwakilishi wa kampuni ya Home Shopping Centre Bi Madiha Al Harthy (kushoto),Salma baada ya kuchangia sh. milioni 22.
Mkurugenzi wa SONGAS Limited Bw;Christopher Ford(katikati),akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya dolla za kimarekani 10,000, mgeni rasmi wa harambee hiyo.kushoto meneja
rasilimali Songas Bi Agatha Keenja.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja (katikati) akipongezwa na Mgeni rasmi wa harambe hiyo baada ya kuchangia sh. 500,000.

eya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 10, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia mpango wa elimu Kata ya Kipawa, iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Fedha hizo zilitolewa na Manispaa hiyo ambapo zaidi ya sh. milioni 400 zilipatikana.
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI Mkuu wa zamani , Edward Lowassa, ameendeleza kuwa mstari wa mbele katika harakati zake za kuchangisha mamilioni ya fedha baada ya kuchangisha Sh.421,850,000 kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Elimu Kata ya Kipawa katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Lowassa ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM), aliendesha harambee hiyo juzi katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Kempiski Jijini Dar es Salaam ambapo yeye mwenyewe alichangia Sh.milioni 10.
Katika harambee hiyo miongoni mwa makampuni yaliyochangia kiasi kikubwa ni Lion Club Sh.milioni 70, Home Shipping Center Sh.milioni 22, African Barrick Gold Dola 10,000, Songas Dola 10,000, Maersk Sea Line ilichangia Sh.Miliono 90, na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja alichangia milioni Sh.10.
Wengine waliochangia ni madiwani, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Chadema, taasisi za watu binafsi na mtu mmoja mmoja ambapo Radio Clauds walitoa muda wa hewani wa kutangaza mpango huo wenye thamani ya sh. milioni 12.
Akizungumza kabla ya kuendesha harambee ya kuchangisha, aliwataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuwahamasisha wananchi kuwekeza katika kuchangia sekta ya elimu.
Lowassa alimpongea Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwa jitihada zake alizozionyesha za kuchangia elimu na kuwataka madiwani wengine kuiga mfano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwaupande wake alisema shule saba za Msingi na Sekondari zilizopo kata hiyo zinakabiliwa na matatizo lukuki ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayosababisha wanafunzi kati ya 140 hadi 160 kusomea katika darasa moja.

“Shule za kata yangu kwa kweli zinakabiliwa na changamoto nyingi, kwa mfano Shule ya Msingi ya Majani ya Chai ina vyumba vya madarasa nane wakati wanafunzi waliopo ni 2,200, Shule ya Msingi ya Minazi Mirefu madarasa yake yaliyopo ni machakavu pia hayatoshelezi,”alisema Kaluwa.
Kaluwa alisema jitihada nyingine zilizofanywa katika kutafuta pesa kwa ajili ya kuziboresha shule hizo ambapo Machi 17 mwaka huu kuliitishwa matembezi ya hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Aliongeza kuwa katika hafla hiyo kiasi cha shilingi milioni 15 kilichangwa na wadau mbalimbali ambapo kati ya hizo Sh.Milioni 3 zilitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Clouds Media Group ambao walitoa shilingi milioni moja na wanafunzi kadhaa wa shule za msingi na sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga aliwashukuru wadau waliojitokeza kuchangia kata hiyo ambayo ipo katika jimbo lake na kuwataka wadau wengeni kuchangia kata zingine ili kukabiliana na matatizo hayo katika shule mbalimbali

Tawi la CHADEMA Washington DC Nchini Marekani Lazidi Kuvuna Wanachama Wapya

Linda Bezuidenhout (LB) furaha baada ya kuvua kamba kuvaa kwanda na kuchukua kadi kuwa mwanachama kamili wa Chama Cha Demokrasia Chadema.
Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe akimkabidhi rasmi mwanacham mkareketwa ambae ni mwana mitindo Linda Bezuidenhout (LB) kati ya uwanachama wa chama cha Demokrasia Chadema katika ofisi ya tawi la Tawi la Chama Washington DC.
Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Kalley Pandukizi akiwa na katibu wachama hicho,Ndugu Libe Mwang'ombe alipotoa kadi rasmi kwa Beautician maharufu na designer wa kitanzan Linda Bezuidenhout (LB)
Viongozi wa tawi la chadema Washington DC wakipata Champagne
Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe wakipata picha ya pamoja na Linda Bezuidenhout Atlanta, Georgia na wanachama wa tawi la chadema Washington DC.
Katika miaka ya nyuma Linda aliwahi kusponsor matukio mbali mbali kwenye miaka ya 1990 wengi wao wakimjua kwa Linda Express Nchini Tanzania ambae ambaye hivisasa anajishughulisha na biashara ya nguo za kiume milanovita.com pamoja na zakike ambazo anadesign mwenyewe kwa brand name ya Linda kutoka Atlanta, Georgia Nchini Marekani.Picha na Mdau Wa Swahilivilla

TANGAZO LA OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA :UPOTEVU WA VITABU ISHIRINI (20) VYA LESENI YA BIASHARA


Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa inapenda kuutangazia Umma kuwa imepotelewa na vitabu ishirini (20) vya leseni za biashara vilivyopotea tarehe 22 Mei 2012 katika moja ya Daladala Jijini Dar es Salaam.
Vitabu hivyo vilivyotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara vikiwa na kumbukumbu namba 1389501 mpaka 1391500.
Kwa yeyote atakayeona vitabu hivyo au kuvinunua anaombwa avipeleke kituo chochote cha polisi kilicho karibu yake au kutoa taarifa juu ya mwenye navyo katika kituo hicho.
Ifahamike kuwa vitabu hivyo ni batili hivyo haviruhusiwi kutumika kwa namna yeyote ile. Na atakayethibitika kuvitumia atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.
Ewe mfanyabiashara, epuka manunuzi na matumizi ya vitabu vyenye namba tajwa hapo juu kwa usalama wa biashara yako.
Kwa mawasiliano tunaomba mtumie namba zetu hapo juu.
Tunaomba ushirikiano wenu.
IMETOLEWA NA
HAMZA TEMBA
AFISA HABARI MKOA WA RUKWA
07/06/2012

YONDAN AKIMWAGA WINO YANGA NA KITITA CHAKE CHA MIL.30

KELVIN Patrick Yondan, beki wa kati wa Simba amekana kusaini mkataba wowote na Simba na amesema yeye amesaini Yanga tu mkataba wa miaka miwili.
Yondan amesema Simba wanampakazia kusaini mkataba mpya na anataka wapenzi wote wa soka Tanzania watambue kwamba kuanzia sasa yeye ni mchezaji halali wa Yanga.
Yondan aliikana Yanga awali kwa sababu walimsainisha fomu bila kumpa fedha, lakini leo amepewa Milioni 30 zake taslimu na amemaliza kila kitu.

TIKA itaboresha huduma Ilala- Meya wa Ilala Jerry Slaa

Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Slaa akufungua semina ya Mpango wa bima ya Afya unaojulikana kama TIKA uliobuniwa na Mfuko wa Bima wa Afya (NHIF) inayotolewa kwa madiwani wa Manispaa hiyo inayofanyika kwenye ukumbi wa Arnautoglo Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam asubuhi hii, kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa NHIF Bw Khamis Mdee na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ellias Mwasabwite.
Naibu Mkurugenzi wa NHIF Bw Khamis Mdeeakizungumza katika semina hiyo kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ellioth Mwasabwite na katikati ni Meya wa Ilala Mh. Jerry Slaa.
Wakurugenzi na maafisa kutoka Mfuko wa Bima wa Afya wakiwa katika semina hiyo leo.
Madwani wanaoshiriki katika semina hiyo wakifuatilia kwa makini mada katika semina hiyo.
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Slaa kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Khamis Mdee na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ellias Mwasabwite.
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Slaa kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Khamis Mdee na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Ellias Mwasabwite.

No comments:

Post a Comment